|
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) |
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO,
kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya –EU- wamejenga kituo cha utamaduni
kitakachotumika kutunza kumbukumbu muhimu za jamii ya kimasai na kutoa
elimu za kitamaduni kwa njia ya kieletroniki katika wilaya ya NGORONGORO
mkoani ARUSHA.
Mwakilishi wa UNESCO nchini, ANNA CONSTANTINE, amesema kituo hicho
kitasaidia kutoa elimu mbali mbali hasa kuhusu namna ya kuhifadhi
tamaduni
Kwa upande wake Mwakilishi toka Umoja wa Ulaya- EU-OLIVIER COUPLEX,
amesema makubaliano yakuanza ujenzi wa mradi huo wa kituo cha utamaduni
ulifikiwa mwaka 2012 baina ya serikali ya TANZANIA na Umoja wa Ulaya
EU.
|
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akimwelezea Katibu
Tawala, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Lemuel Kristian Kileo (wa
pili kushoto), namna mradi wa ujenzi wa kituo cha sanaa. |
Mkuu wa mkoa wa ARUSHA, MRISHO GAMBO, amelishukuru shirika la UNESCO
pamoja na Umoja wa ulaya EU kwa jitihada mbali mbali za kuleta maendeleo
nchini na pia amesema kituo hicho kitasaidia kutunza kumbukumbu muhimu
kuhusu tamaduni za maasai kutokana na jamii hiyo kuwa na tamaduni
nyingi ambazo zimekuwa kivutio kikubwa ndani na nje ya nchi.