Sunday, October 30, 2016

Watu Wawili wahukumiwa kifo kutokana na mauaji ya binti mwenye ualbino



Mahakama kuu kanda ya BUKOBA imetoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa LAMECK BAZIL na PANCRAS MINAGO baada ya kupatikana na hatia ya kula njama na kumuua kwa kukusudia marehemu  MAGDALENA ANDREA ambaye alikuwa na ualbino.

Watu hao walifanya kosa hilo mwaka 2008 katika wilaya ya BIHARAMULO Mkoani KAGERA na hukumu ya kesi hiyo namba 57 ya mwaka 2015 inaweka rekodi kwa kuwa kesi ya kwanza katika mahakama kuu kanda ya BUKOBA kutoa  adhabu ya kifo dhidi ya watu waliotenda kosa la mauaji kwa watu wenye ualbino.


Mnamo Septemba 21 mwaka 2008 katika kijiji cha LUSABYA katika kata ya RUNAZI wilayani BIHARAMULO Mkoani KAGERA, LAMECK BAZIL ambaye ni mganga wa jadi mwenyeji wa mkoa wa MARA ambaye alifika kijijini hapo kwa shughuli za utabibu alimshawishi baba mkwe wake PANCRAS MINAGO kumshambulia na kisha kumuua  MAGDALENA ANDREA kwa lengo la kunyofoa baadhi ya viungo vyake ili kwenda kuviuza.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com