Sunday, October 30, 2016

MACHINGA watakiwa kuondoka maeneo yasiyo rasmi


Mkuu wa mkoa wa DAR ES SALAAM, - PAUL MAKONDA ametoa muda siku 14 kwa wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kuandaa maeneo

Mkuu wa mkoa wa DAR ES SALAAM, - PAUL MAKONDA ametoa  muda siku 14  kwa wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kuandaa maeneo ya kufanyiabiashara   kwa wafanyabiashara wadogo maarufu kama MACHINGA.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini DAR ES SALAAM, - MAKONDA  amepiga marufuku wafanyabiashara hao kufanya shughuli zao maeneo yasiyo rasmi.
MAKONDA amesema kuwa wafanyabiashara hao wadogo  wanatakiwa kufanya biashara  zao katika  maeneo rasmi na si kando ya barabara na  pembezoni mwa maduka, na pia amewataka kuacha kutumia  vibaya ruhusa ya Rais JOHN MAGUFULI aliyetaka kutobughudhiwa kwa Wafanyabiashara hao wadogo


0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com