Featured
Showing posts with label sport. Show all posts
Showing posts with label sport. Show all posts

Thursday, May 25, 2017

SportPesa Super Cup Kuieleta Timu ya Everton Bongo




Najua inawezekana ukawa na shauku ya kuona michuano ya SportPesa Super Cup inafanyika mapema zaidi kutokana na upendo wako na soka baada ya kusikia kuwa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sport Pesa imeanzisha mashindano hayo na yataanza June 5 hadi June 11 2017.
Good news nyingine iliyoritipotiwa leo na moja kati ya mitandao mikubwa England ni kuhusiana na club ya Everton kuwa itakuja Tanzania na Alhamisi ya July 13 itacheza mchezo mmoja wa kirafiki na moja kati ya timu nane zitakazoshiriki michuano ya SportPesa Super Cup.





Mtandao wa liverpoolecho.co.uk ndio umeripoti taarifa hizi huku ikithibitisha kuwa timu za Simba, Yanga, Singida United, Jang’ombe Boys, AFC Leopards, Tusker FC, Gor Mahia na Nakuru All Stars ndio zitashiriki michuano hiyo na moja kati ya timu hizo itacheza na Everton.


ame ya Everton itakuwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam na ujio wao Tanzania ni sehemu yao ya makubaliano yao ya udhamini na SportPesa, mtandao wa liverpoolecho.co.uk ni moja kati ya mitandao mikubwa katika jiji la Liverpool ambapo inatokea timu ya Everton.

Sunday, May 14, 2017

Hiki Ndicho Alichosema MO kwa simba




Baada ya  simba na SportPesa Tanzania rasmi  kutangza udhamini wake wa miaka mitano kwa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, wenye thamani ya Sh. Bilioni 4.96.

MO kawaandikia Simba ‘demand note’ kwa kua wamekiuka makubaliano yao kwamba, atoe pesa kama makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba inabidi wakae meza moja viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba, lakini viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya.

Simba ilishaanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokua ombi la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama wakibaki na hasilimia 49.
Adi kufikia leo akuna majibu yoyote yaliotoka simba na hiki ndicho alichokiandika Mo kwenye hukurasa wake wa instagram



"Inasikitisha kuwa uongozi wa Klabu ya Simba umesaini mkataba wa udhamini wa muda mrefu bila kunishirikisha. Kwa muda mrefu nimeweka nguvu zangu kwenye klabu."


Saturday, May 13, 2017

Waspania wa Mkubali Farid Mussa Malik na wakisema hiki


MAKOCHA wa timu ya vijana ya Deportivo Tenerife wamemuambia winga wa kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa hana muda mrefu kabla ya kuanza kucheza Ligi kubwa Ulaya.


Hiyo inafuatia makocha hao kuvutiwa na kiwango cha mchezaji huyo katika mechi zake za timu ya vijana DC Tenerife ya Hispania.

Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online kwa simu leo kutoka Hispania, Farid amesema kwamba juzi baada ya kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao katika ushindi wa 5-1 Uwanja wa Heliodoro Rodriguez walimpongeza sana na kumuambia atafika mbali.

“Juzi nilifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao, baada ya mechi wakanifuata kwa furaha na kuniambia mimi ni mchezaji mkubwa wa baadaye, sina muda mrefu nitacheza ligi kubwa. Kwa kweli imenifariji sana na kunitia moto wa kujituma zaidi,”amesema Farid.

Kwa wiki hii peke yake, Farid amefikisha mabao matatu baada ya Jumatatu kufunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao katika ushindi wa 3-0.

Farid alijiunga na klabu hiyo ya Santa Cruz de Tenerife, Tenerife, visiwa vya Canary Desemba mwaka jana kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.
Azam FC ilimtoa kwa mkopo Farid kwenda CD Tenerife kwa makubaliano maalum baada ya winga huyo kufuzu majaribio katika klabu hiyo Aprili mwaka jana alipokwenda na Mkurugenzi wa klabu yake, Yussuf Bakhresa.

Farid alitua Hispania kwa mara ya kwanza Aprili 21, mwaka jana baada ya kuichezea Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance mjini Tunis, Tunisia ikifungwa 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.


Na ilimchukua wiki moja tu Farid kuwakuna kwa kipaji chake makocha wa Tenerife na kutaka kumnunua, lakini Azam ikakataa na kuamua kumtoa kwa mkopo Desemba, 2016.


Na baada ya kutua Tenerife akapangiwa kuanza kuchezea kikosi cha U-20 ili kupata uzoefu kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza kinachocheza Segunda, Ligi ya pili kwa ukubwa Hispania.

Wednesday, May 10, 2017

HIMID MAO APEWA DAKIKA 90 DENMARK TIMU YAKE YAPIGWA 2-0


 Himid Mao Mkami leo amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba na timu ya Randers FC ya Denmark na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Horsens.

Kiungo huyo wa Azam FC ya Dar es Salaam ambaye yupo Denmark kwa majaribio ya kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu, amecheza kwa dakika zote 90 na kwa bahati mbaya wachezaji wa akiba wa Randers FC wakafungwa 2-0.


" Himid amesema kwamba ulikuwa mchezo mgumu, lakini upande wake anamshukuru Mungu amecheza vizuri."

“Unajua kufungwa haimaanishi mmecheza vibaya, wakati mwingine mnaweza kucheza vizuri kuliko waliowafunga, sema basi tu mambo ya mpira,”amesema Himid, mtoto wa kiungo wa zamani wa Pamba, Mao Mkami ‘Ball Dancer’.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania amesema baada ya kufanya mazoezi na timu hiyo kwa takriban siku tatu na leo kucheza mechi ya kwanza – kesho anatarajiwa kupewa ratiba mpya.


Himid amesema anaamini baada ya kucheza Tanzania kwa muda mrefu, sasa ni wakati mwafaka kwake kutoka nje.
“Ni kweli nina nia sana ya kutoka nje kwa sasa, naamini ni wakati mwafaka kwangu kupata changamoto mpya katika maisha yangu ya soka,”amesema Nahodha huyo Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.   

Wednesday, May 3, 2017

Viongozi kutoka Ukanda wa CECAFA wakubaliana kuimarisha soka



Marais kutoka mataifa yanayounda Baraza la soka Afrika Mashariki CECAFA, walikutana jijini Kampala nchini Uganda siku ya Jumatano kuzungumzia namna ya kuboresha mchezo wa soka katika ukanda huo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na marais saba wakiongozwa na mwenyeji wao Moses Magogo, Vincent Nzamwita kutoka Rwanda, Jamal Malinzi (Tanzania), Juneidi Tilmo (Ethiopia), Nicolas Mwendwa (Kenya) na Ndikuniyo Reverien (Burundi).
Ravia Faina rais wa Shirikisho la soka kutoka kisiwa cha Zanzibar kilichopewa uanachama wa CAF hivi karibuni, pia alikuwepo.
Mambo saba yaliyoafikiwa katika mkutano huo ni pamoja na:-
1 – Kuibadilisha Katiba ya CECAFA.
2 – Kuandaa mkutano mkuu wa CECAFA haraka iwezekanavyo.
3 – Kuhakikisha kuwa CECAFA inapata Makao makuu ya kudumu.
4 – Kuimarisha michuano ya vijana wasiozidi miaka 15, 17 na 20 kwa wavulana na wasichana pamoja na kuboresha soka la ufukweni.
5 – Kuimarisha hali ya waamuzi uwanjani, makocha, uongozi lakini pia hali ya matibabu kwa wachezaji.
6 – Kuimarisha mawasiliano na kuitangaza CECAFA.
7 – CECAFA kuomba nafasi ya kuandaa fainali ya mataifa bingwa barani Afrika katika siku zijazo.
8 –CECAFA kuwakilishwa ipasavyo katika Kamati kuu ya CAF.
9 –Kuja na mbinu za kuandika mapendekezo kwa Shirikisho la soka duniani FIFA ili kusaidia kuinua soka la vijana, wanawake na lile la ufukweni.

Mkwasa asema aina mpango wa kuwatema wachezaji Yanga


Bonifasi Mkwasa Katibu Mkuu wa Yanga

Katibu Mkuu wa Yanga SC,  Charles Boniface Mkwasa amekanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba wana nia ya kuwaacha baadhi ya wachezaji wake na kusema hizo taarifa na uzushi mkubwa ndani ya klabu yao.


Mkwasa amebainisha hayo kupitia taarifa yake aliyoitoa asubuhi ya leo baada ya kuenea kwa taarifa kutoka baadhi ya vituo vya Radio na 'social network' zikidai klabu hiyo inataka kuwabwaga baadhi ya wachezaji wake kutokana na kufanya vibaya katika Ligi.
"Taarifa hizo ni za uongo na uzushi mkubwa, uongozi upo bega kwa bega na wachezaji wote 27 na benchi la ufundi. Hatujakaa kulijadili hilo wala kulifikiria bali tupo makini kutetea ubingwa wetu wa ligi kuu". Alisema Mkwasa
Aidha, Mkwasa alisisitiza kwamba Kocha Mkuu, George Lwandamina ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho juu ya huduma ya wachezaji ndani ya klabu hiyo na wala siyo kiongozi mwingine yoyote
"Kocha Mkuu George Lwandamina hajatoa taarifa yoyote ya kumwacha mchezaji gani au yupi wa kumuongezea mkataba,  zaidi ya kila siku kuukazia uongozi kuboresha masilahi ya wachezaji kwa sababu kama kocha mkuu anajivunia na kujali kazi ya vijana wake". 

Himid aka Niinja kwenda Ulaya kutafuta maisha ya soka la kulipwa


himid mao akiwa Denmark ndani ya uwanja wa timu ya Randers FC

Kiungo wa Azam FC  na timu ya taifa ya Tanzania Himid Mao ameondoka nchini jioni ya leo Mei 1, 2017 kuelekea Denmark kwa ajili ya majaribio ya kutafuta kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Himid anakwenda kwenye klabu ya Randers FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo ligi inayojulikana kwa jina la Superliga.

Kiungo huyo ameonesha kiwango cha juu katika msimu huu kuanzia kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara, kombe la Azam Sports Federation Cup, michuano ya kimataifa pamoja na mechi za timu ya taifa.shaffihdauda.co.tz ilizungumza na Himid Mao muda mfupi kabla hajaondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Nyerere.
“Naenda kwenye klabu ya Randers FC ya nchini Denmark kwa ajili ya majaribio kwa muda wa siku 15, kama mchezaji najiamini naweza kufanya lolote sehemu yoyote, mambo mengine ya mbeleanajua Mungu,” amesema Himid muda mfupi kabla ya kuondoka ardhi ya Bongo.

“Mimi wajibu wangu ni kujitolea kadiri niwezavyo na kuwashawishi hao kwa uwezo wangu wote patakapobakia ni kazi ya Mungu.”
“Kila kitu kipo kama kilivyopangwa, klabu yangu inajua, wakala anajua kwa hiyo kila kitu kipo wazi utakapofika wakati wa klabu kutangaza chochote watafanya hivyo.”

“Kwa sasa naangalia hiki kilichopo mbele halafu baadae tutajua nini kitakachofuata.”

Tuesday, March 14, 2017

Kiokosi kipya cha Taifa Stars 2017




Kocha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga ametangaza majina 26 ya wachezaji watakaounda kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya kufuzu kucheza michuano ya CHAN pamoja na ile ya AFCON.
Magolikipa: Aishi Manula (Azam), Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Mabeki: Shomary Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Yanga), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba), Gadiel Michael (Azam), Andrew Vincent (Yanga), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam FC).
Viungo: Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Said Ndemla (Simba), Frank Domayo (Azam), Muzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (DC Tennerife) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden), Ibrahim Hajib (Simba), Mbarak Yussuf (Kagera Sugar) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).
Stars itaingia kambini Machi 19 mjini Dar es Salaam na itacheza mechi mbili za kirafiki za kujipima nguvu.
Mechi hizo zitachezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Botswana Machi 25 na Burundi Machi 28.

Taifa Stars itaanza na Rwanda katika kuwania tiketi ya CHAN mwakani nchni Kenya na mechi ya kwanza itachezwa Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kati ya Julai 14 na 16 kabla ya timu hizo kurudiana Uwanja wa Amahoro, Kigali kati ya Julai 21 na 23.
Ikifanikiwa kuitoa Rwanda, Tanzania itamenyana na mshindi kati ya Uganda na ama Sudan Kusini au Somalia katika Raundi ya Tatu ya mchujo mechi ya kwanza ikichezwa kati ya Agosti 11, 12 na 13 na marudiano kati ya Agosti

Monday, February 6, 2017

Mtanzania anayecheza soka PSG ya Ufaransa




Mtanzania Haytham Saduun ameeleza safari yake ya soka ilivyokuwa kutoka Bongo hadi kufika kwenye academy ya PSG ya Ufaransa moja kati ya vilabu vikubwa barani Ulaya.
Haytham ambaye kwa sasa anamiaka 18, safari yake ya soka imeanzia katika timu ya vijana ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro ambapo alikuwa anakipiga kabla ya kwenda Uarabuni kwa matembezi kisha kutumia fursa hiyo kusonga mbele zaidi.
Kijana huyo anaetokea maeneo ya Temeke-Mwisho (Kitomondo au Wailes) anasema alipata safasi ya matembezi kwenda Oman ambapo wakati yupo huko alipata fursa ya kucheza kwenye academy ya Muscat akaonesha uwezo wakamuhitaji na kumpa muda zaidi.


Safari ilivyoanza
“Nilipata nafasi ya kwenda Urabuni (Oman) nikapata nafasi ya kucheza academy ya Muscat baada ya kufanyiwa trial kwa siku tatu. Kulikuwa na safari ya kwenda Dubai kwa ajili ya mashindano ya Dubai Super Cup, tulicheza mashindano yale na kufanikiwa kuchukua ubingwa huku mimi nikifanikiwa kufunga magoli matatu katika michuno hiyo na kuonesha kiwango kizuri,”-Haytham.


Dili la PSG linaibuka
Kulikuwa na ma-scout mbalimbali kutoka nchi za Ulaya, alikuwepo pia muwakilishi kutoka Ufaransa ambaye alinihitaji kwa sababu alianza kunifatilia tangu nikiwa academy (Muscat, Oman).
Alinifanyia mipango ya kunipeleka Paris St Germain baada ya kila kitu kukamilika tukaenda pamoja na wenzangu wengine kwa ujumla tulikuwa watu sita. Tukafanya trial kwa muda wa siku tano na bahati nzuri nikafanikiwa kufuzu mimi pekeangu.

Imepata sponsorship ya kuingia professional kwa hiyo mwaka huu kama Mungu akipenda naweza nikafika hapo kutokana na mipango inayofanyika sasa hivi


Vipi kuhusu kuitumikia Tanzania?
Nilipata nafasi ya kubadilisha uraia lakini uongozi wangu ukakataa kwa sababu tuna kauli yetu moja inaitwa ‘Tanzania Kwanza’. Mimi nipo tayari kujitolea kuitumikia nchi yang na kuitangaza hata kama ningekuwa na mguu mmoja nikiitwa timu ya taifa nitakuwa tayari.

Ushauri kwa vijana wa kibongo
Nimepitia mambo mengi magumu sana katika harakati zangu, lakini kumuweka Mungu mbele ni muhimu sana. Hapa nyumbani ushirikina umewekwa mbele sana lakini uchawi kwenye mpira ni mazoezi, jitihada binafsi na nia.

Hakuna kinachoshindikana chini ya jua, nitajitahidi na kuongeza nguvu zaidi na kufanya kila kinachowezekana huku nikiweka mbele malengo yangu ya kufika sehemu ninayotaka, natamani kuwa mchezaji wa kwanza kucheza ligi kuu ya Ufaransa.

Saturday, January 21, 2017

ULIMWENGU KUTIMKIA LIGI KUU YA SWEDEN MIAKA MIWILI




MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu anaondoka nchini leo kwenda kukamilisha usajili wake klabu ya AFC Eskilstuna ya Ligi Kuu ya Sweden.

Akizungumza na Bin Chombo kimoja cha habari Sports – Online leo, Ulimwengu amesema kwamba baada ya mazungumzo ya awali na klabu hiyo anakwenda kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, ambayo awali ilikuwa inajulikana kama FC Cafe Opera na Vasby United.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa watu wangu wote wa karibu kama Jamal Kisongo ambao wamekuwa karibu na mimi kwa kipindi chote hiki na kunipa ushauri hadi kufikia maamuzi haya ya kujiunga na timu hii. Tumekataa ofa nyingi sana na kuikubali hii kwa sababu za msingi sana,”alisema.

“Kila kitu ni malengo tu, inategemea na mtu unataka kitu gani katika wakati gani, nakwenda AFC Eskilstuna kucheza mpira kama nilivyocheza TP Mazembe ili nionekane nisogee mbele zaidi,”alisema.

Ulimwengu aliyezaliwa Juni 14, mwaka 1993 aliibukia katika taasisi ya soka Tanzania (TSA) mwaka 2008, kabla ya mwaka 2009 kwenda kuanza kukomazwa Ligi Kuu katika klabu ya Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi mwaka 2010 alipokwenda akademi ya Athletic FC ya Sweden, alikocheza hadi 2011 TP Mazembe alipochukuliwa na timu ya vijana ya Mazembe.


Alicheza U-20 ya Mazembe kwa msimu moja kabla ya kupandishwa rasmi timu ya wakubwa mwaka 2012 na moja kwa moja kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza hadi anamaliza Mkataba wake Oktoba mwaka jana.

Ulimwengu anajivunia kushinda mataji makubwa akiwa na  Mazembe kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Super Cup ya Afrika na pamoja na kucheza Klabu Bingwa ya Dunia.

Ulimwengu alisema kwamba anashukuru Mungu ndoto zake za kucheza Ligi Kuu Ulaya zinatimia na ataitumia AFC Eskilstuna kama daraja la kupandia timu kubwa barani humo.

Wednesday, January 18, 2017

Okwi avunja mkataba na Sonderjyske Fodbold, Kurejea Simba?


Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda,  Emmanuel Okwi ameachana rasmi na klabu ya  Sonderjyske Fodbold ya Denmark kwa makubaliano ya pande zote kuamua kusitisha mkataba.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Danish Superliga Jorgen Haysen uamuzi huo umefikiwa baada ya Okwi kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.
“Okwi hakuwa anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi chetu, na matumaini ya kupata nafasi yamekuwa ya chini sana. Matokeo yake tumekubaliana kububja mkataba, tunamtakia kila la kheri huko mbeleni.’
Klabu hiyo ilimsaini Okwi mnamo July 2015 kwa mkataba wa miaka 5 akitokea klabu ya Simba SC ya Tanzania bara.
Katika dirisha la usajili lililopita kulikuwa na taarifa kwamba mchezaji huyo alikuwa njiani kurejea Msimbazi, hata hivyo ilishindikana kutokana na ada ya usajili waliyokuwa wanataka Sonderjyske Fodbold. 

Monday, January 16, 2017

CAF YAIPA NAFASI YA UPENDELEO CONGO



Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF), limetoa nafasi ya mwisho kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Congo (FECOFOOT) kumpeleka mchezaji Langa Lesse Bercy jijini Libreville, Gabon kwa ajili ya kipimo kipya cha MRI ili kutambua umri wake.

CAF limetaka FECOFOOT kumpeleka mchezaji huyo huko Libreville, Gabon ndani ya siku 10 zijazo kuanzia jana Januari 12, 2017.

CAF limepata kumwita mchezaji huyo mara mbili mwaka jana, na FECOFOOT imeshindwa kumpeleka kwa sababu mbalimbali wanazozijua FECOFOOT.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya kimataifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, vijana waliohitajika kucheza ni wale wenye umri wa chini ya miaka 17.

Langa Lesse Bercy, amelalamikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwamba amezidi umri hivyo kuhitajika kumpeleka kwani hakustahili kucheza hatua ya kufuzu kwa michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.

Fainali za vijana zinatarajiwa kufanyika katika nchi nyingine itakayotangazwa hapo baadaye baada ya Madagascar kuondolewa kuandaa fainali hizo baada ya kubainika kutokamilisha baadhi ya taratibu.

Hii inatokana na ripoti ambayo CAF wameipata kutoka kwa wakaguzi wa maandalizi ya fainali hizo. CAF imefungua kandarasi ya kwa nchi wanachama wengine kuandaa fainali hizo. Mwisho wa kupokea maombi ni Januari 30, mwaka huu.

Kadhalika Kamati ya Utendaji ya CAF, imemteua Rais wa zamani wa TFF, Leodegar Chilla Tenga kuwania nafasi ya uwakilishi katika Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Katika nafasi hiyo kutoka nchi za Afrika zinazozungumza Kiingereza, Tenga atachuana na Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zambia, Kalusha Bwalya na Kwesi Nyantakyi wa Ghana.

Wengine waliopitishwa kuwania nafasi ya uwakilishi katika Kamati ya Utendaji ya FIFA kutoka nchi za Afrika ni Tarek Bouchamaoui wa Tunisia ambaye anaingia kwenye kundi la nchi zinazozungumza lugha za Kiarabu, Kireno na Kihispaniola.


Kwa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa wamo Constant Omari Selemani wa DR Congo na Augustin Sidy Diallo wa Cote d’Ivoire wakati nafasi nyingine za wazi ihuhusisha mwanamke mmoja, wamo Almamy Kabele Camara (Guinea), Chabur Goc (South Sudan), Danny Jordaan (Afrika Kusini), Hani Abo Rida (Misri) na Lydia Nsekera (Burundi).

Tuesday, January 10, 2017

Azam yamtambulisha kocha mpya raia wa Romania


Klabu ya Azam FC imemshusha kocha mpya anaejulikana kwa jina la Aristica Cioaba kutoka Romania.
Kocha huyo amepewa mkataba wa miezi sita kwa ajili ya matazamio kama atafanya vizuri huenda akapewa mkataba wa muda mrefu lakini kinyume na hapo atafata nyayo za akina Zeben Hernandez.
Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd amesema Aristica Cioaba atasaidiwa na makocha wazalendo ambao wanaiongoza Azam kwa sasa wakiongozwa na Idd Cheche.
“Tumeshapata kocha mpya kutoka Romania ambaye tumempa mkataba wa miezi sita ili tuweze kuangalia uwezo wake. Kama atafanya vizuri basi tunaweza kumuongezea muda,” anasema Jafar Idd uku akiziua tetesi za makocha wazawa kujiunga na Azam.
“Kwa sasa atakuwa akisaidiwa na makocha wetu wazalendo ambao wapo na timu wakiongozwa na Idd Cheche.”
Baada ya Zeben na wasaidizi wake kutimuliwa, ziliibuka tetesi kuwa huenda Karl Ongala ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo akiwa mchezaji na kocha msaidizi akarejeshwa kwenye benchi la ufundi la Azam FC.

Mkwasa pia ni miongoni mwa makocha waliotajwa kupewa jukumu la kuinoa Azam baada ya kuachana na timu ya taifa ya Tanzania lakini ujio wa Aristica Cioaba unamaliza tetesi hizo.

Tuesday, January 3, 2017

Thomas Ulimwengu Kwenda Uholanzi


Klabu moja kutoka Uholanzi inatarajia kuleta ofa kesho ya kumuhitaji mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),Thomas Ulimwengu.

Wakala wa Ulimwengu, Jamal Kisongo, amesema kwa sasa asingeweza kuitaja timu hiyo, hadi siku ya Jumatano, pamoja na ofa nyingine, zilizopo mezani hadi sasa.

Kisongo amesema kuna matarajio ya Ulimwengu kupata timu Ulaya na amewataka Watanzania wawe wavumilivu na kumuombea kijana huyo, ili afanikiwe kucheza Ulaya.

Ulimwengu, na Mbwana Samatta anayecheza Ubelgiji kwa sasa kwenye klabu ya Genk, tangu mwezi wa Januari mwaka uliopita, wote walikuwa wakiichezea TP Mazembe ya DR Congo kabla ya kumaliza mikataba yao mwaka uliopita. 

BREAK NEWSKOCHA MPYA WA TAIFA STARS




Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda  (Interim coach), wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.

Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.
Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).


TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.

Monday, January 2, 2017

HAJIB: KUPATA SHAVU KUTOKA TIMU TATU



MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Hajib Migomba amerejea nchini jana na kusema kwamba atajiunga na timu itakayompa ofa nzuri kati ya Haras El Hodoud ya Misri na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo baada ya kuwasili nchini kutoka Misri alipokwenda kufanya majaribio klabu ya Haras El Hodoud, Hajib amesema kwamba anaweka mbele maslahi katika kuamua timu ya kujiunga nayo.

Pamoja na kufuzu majaribio na vipimo vya afya Haras El Hodoud, lakini imeripotiwa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini pia inatamaka mchezaji huyo wa Simba kwa kusaini naye mkataba moja kwa moja bila majaribio.

Kuhusu Haras, Hajib amesema kwamba amefanya mazungumzo ya awali na Haras El Hodoud na kufikia makubaliano, lakini kwanza wanatakiwa kumalizana na klabu yake ya sasa, Simba SC.

“Ninamshukuru Mungu nimefurahia siku zangu chache za kuwa Alexandria, nilikuwa katika klabu nzuri, mazingira mazuri na wachezaji wenzangu kule wamenikubali mapema sana. Sasa baada ya yote, ninawasikilizia wao tu ni jinsi gani watalimalizia hili suala,”amesema.

Kwa upande wake, Katibu wa Simba, Patrick Kahemele amesema klabu haijapokea ofa yoyote kutoka Haras El Hodoud wala taarifa ya majibu ya majaribio ya mchezaji. “Sisi wenyewe tunasikia tu kutoka kwenye vyombo vya habari kwamba Hajib kafuzu. Kwa hiyo tunasubiri majibu rasmi,”amesema. 


Wakala anayeshughulikia mipango ya Hajib nchini Afrika Kusini, Rodgers Mathaba kwa upande wake alikiri juu ya mchezaji huyo kutakiwa na Kaizer Chiefs.


“Ni kweli, Kaizer wanamtaka Hajib. Najua alikuwa Misri, nasubiri arejee Dar es Salaam nimpigie simu nizungumze naye. Tayari nimekwishazungumza na kocha Steve Khompela wa Kaizer,”alisema.

Hajib alikuwa ana wiki nzuri ya majaribio Haras El Hodoud ikiwemo kufunga bao moja katika ushindi wa 4-0 kwenye mchezo wa kirafiki Ijumaa.

Mathaba ndiye aliyempeleka Hajib Afrika Kusini kwa majaribio pia, klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Ligi Kuu ya ABSA nchini humo na pamoja na kufuzu, wakamtaka arejee Simba kumalizia Mkataba ili baadaye aende kama mchezaji huru.


Lakini sasa mambo yamebadilika na klabu za Afrika Kusini na Misri zipo tayari kumnunua Hajib kutoka Simba.   



Na akizungumzia hilo, Hajib amesema; “Ni kweli nimesikia hizo habari, na si Kaizer tu, timu nyingine kama mbili za Afrika Kusini nazo zimetangaza ofa. Kwanza ninamshukuru Mungu. Mungu ni mkubwa, sasa tusubiri haya maneno yawe vitendo ndiyo tufanye maamuzi,”.

Thursday, December 29, 2016

WA MISRI, WAARABU WAKOLEA...SASA WATAKA KUONGEA BIASHARA NA SIMBA


MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Hajib Migomba amefuzu majaribio katika klabu ya Haras El Hodoud ya Ligi Kuu ya Misri.

Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo kutoka mjini Alexandria yalipo makao makuu ya timu hiyo, Hajib alisema kwamba leo ameambiwa amefuzu majaribio yake baada ya siku tano.
"Nimepewa majibu kwamba nimefuzu, kwa hiyo kinachofuata ni hii klabu kuzungumza na Simba ili wakubaliane kwanza, ndipo nitajua mustakabali wangu,"amesema Hajib.  


Hajib aliondoka Alhamisi iliyopita nchini kwenda Misri kwa majaribio ya kucheza soka ya kulipwa baada ya kupewa baraka zote na uongozi wa Simba. 

Mshambuliaji huyo ameonyesha kiu ya kweli ya kutaka kucheza nje ya Tanzania, kwani katikati ya mwaka huu alikwenda Afrika Kusini kwa majaribio pia, ambako pamoja na kuripotiwa kufuzu katika klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Ligi Kuu ya ABSA nchini humo. 

Azam FC, Imevunja Mkataba na makocha Hispania



UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuufahamisha umma kuwa umefikia makubaliano ya pande mbili ya kusitisha mikabata ya makocha wake kutoka nchini Hispania.

Jopo hilo la makocha linaundwa na Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Msaidizi wake, Yeray Romero, Kocha wa Makipa Jose Garcia, Kocha wa Viungo, Pablo Borges na Mtaalamu wa tiba za Viungo, Sergio Perez.
\
Uamuzi huo umefikiwa na Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo jana, na umetokana na mwenendo mbaya wa Azam FC kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), ambayo imefikia raundi ya pili hivi sasa.

Azam FC inawatakia kila la kheri na mafanikio mema makocha hao huko waendako na inawashukuru kwa mchango wao wote walioutoa kwenye timu kwa kipindi chote walichokaa, ikiwemo kuwapa taji la kwanza la Ngao ya Jamii mwaka huu kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare ya mabao 2-2.

Wakati huu ambapo uongozi wa Azam FC upo katika mchakato wa kusaka kocha mpya, kikosi hicho kitakuwa chini ya makocha wa timu ya vijana ya timu hiyo, Idd Cheche na Kocha wa Makipa, Idd Abubakar, ambao walianza kazi jana jioni kukiandaa kikosi kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons.

Azam FC inapenda kuwaambia mashabiki wake kuwa wawe watulivu katika kipindi hiki kwani uongozi umefanya uamuzi sahihi kwa ajili ya kuinyanyua timu juu ili hatimaye ushiriki wetu wa michuano mbalimbali uweze kuwa ni wa kiwango cha juu tofauti na hali ilivyokuwa sasa.


Hernandez anaondoka Azam FC akiwa ameingoza timu hiyo kwenye mechi 18 rasmi ambazo ni za mashindano, 17 za ligi na moja ya Ngao ya Jamii, amefanikiwa kushinda mechi nane, sare sita na kufungwa mara nne.

Friday, November 25, 2016

LWANDAMINA AKABIDHIWA TIMU RASMI LEO NAKUSMA HAYA..


Geroge Lwandamina ametambulishwa rasmi kuwa kocha mpya wa Yanga SC akirithi nafasi ya kocha wa zamani wa klabu hiyo Hans van der Pluijm ambaye amepewa majukumu mapya ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi ndani ya klabu hiyo inayotetea ubingwa wake wa VPL ilioutwaa msimu uliopita.
|"amesema kwamba atafanya kazi na Maofisa aliowakuta benchi la Ufundi na hataleta mtu mpya.Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam wakati wa utambulisho wa wakuu wapya wa Idara ya Ufundi, Lwandamina alisema kwamba hana mpango wa kubadilisha chochote kwenye benchi la Ufundi.Na kuhusu kuongeza wachezaji, Lwandamina amesema kwamba ameiona Yanga katika mechi yake ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikishinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting na amegundua "ni timu nzuri ambayo haihitaji mchezaji mpya.
Lwandamina amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomuweka Jangwani.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amewatambulisha wawili hao ndani ya makao makuu ya klabu ya Yanga na kumkabidhi Lwandamina jezi ya Yanga ikiwa ni ishara ya utambulisho na kumkaribisha ndani ya klabu.

Pluijm pia ametangazwa rasmi kuchukua majukumu mapya ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi akiachana na masuala ya ukocha ndani ya klabu hiyo aliyoipa mafanikio makubwa ikiwa chini yake kama kocha mkuu.

Lwandamina amekabidhiwa klabu ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara pointi mbili nyuma ya vinara wa ligi Simba ambao wanapointi 35 baada ya mzunguko wa kwanza kumalizika.

Kocha huyo (Lwandamina) aliifikisha Zesco United hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika msimu uliomalizika hivi karibuni, atakuwa na kibarua kuhakikisha anatetea taji la VPL, Azam Sports Federationa Cup (FA Cup) pamoja na kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa ambapo msimu uliopita ilifika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika chini ya Pluijm.

Kocha huyo mpya wa yanga akitoa sifa kemukemu:

Alimsifu mtangulizi wake, Pluijm kwamba amefanya kazi nzuri na akasema atafuata nyayo zake na atashirikiana naye bega kwa bega kuhakikisha Yanga inapata mafanikio zaidi.
Lwandamina amekana madai kwamba amependekeza wachezaji wawili aliokuwa nao Zesco United ya kwao, Zambia kiungo Misheck Chaila na mshambuliaji Mkenya Jesse Were wasajiliwe pia. 
Baada ya kuiongoza Yanga katika jumla ya mechi 128 kwenye awamu mbili, akishinda 80, sare 25 na kufungwa 23, Pluijm aliyetua Jangwani mwaka 2014 anampisha Lwandamina.
Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 110 za tangu mwaka jana, alishinda 69, sare 19 na kufungwa 21.
Na anahama nafasi baada ya msimu mzuri uliopita, akibeba mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC).
Pluijm pia aliiwezesha Yanga kufika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika (Kombe la Shirikisho) kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 na mara ya pili kihistoria. Yanga ilifika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu baada ya mwaka 1998 kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
Na kwa mafanikio hayo, haikuwa ajabu Pluijm akishinda tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu uliopita. 
Benchi jipya la Ufundi Yanga sasa linakuwa chini ya Pluijm kama Mkurugenzi, Lwandamina Kocha Mkuu, Juma Mwambusi Kocha Msaidizi, Juma Pondamali Kocha wa makipa, Hafidh Saleh Meneja, Daktari Edward Bavu, Jacob Onyango Mchua Misiliu na Mtunza Vifaa Mohamed Omar ‘Mpogolo’.



YANGA YA KABIDHIWA RASMI ENEO LA KUJENGA UWANJA....




Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Bw. Yusuph Manji ameikabidhi Yanga eneo la ekari 715 lililopo maeneo ya Gezaulole, Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa klabu hiyo pamoja na kituo maalum cha kukuza vipaji vya michezo.

Wasaidizi wa Manji walikabidhi eneo hilo kwa Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa klabu hiyo mama Fatma Karume katika hafla fupi ambayo pia ilihudhuriwa na Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba.

Wasaidizi wa Manji walikabidhi eneo hilo jana mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na maofisa wa serikali ya Kigamboni.

Mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa Yanga, Fatma Karume ndiye aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu ambapo pia walikuwepo Dk Jabir Katundu, ambaye ni mjumbe wa baraza la wadhamini, mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Samuel Lukumay na Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit.

Manji amekabidhi eneo hilo ikiwa ana hesabu kadhaa zilizosalia kabla hajakabidhiwa timu baada ya mechi ya keshokutwa.


Baada ya kukabidhiwa eneo hilo, wadhamini wa klabu hiyo wanatarajia kulitambulisha rasmi kwa wanachama wao wiki ijayo. Eneo hilo lina ekari 715 ikiwa ni ukubwa zaidi ya eneo lililojenga Uwanja wa Uhuru.

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com