Friday, November 25, 2016

YANGA YA KABIDHIWA RASMI ENEO LA KUJENGA UWANJA....




Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Bw. Yusuph Manji ameikabidhi Yanga eneo la ekari 715 lililopo maeneo ya Gezaulole, Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa klabu hiyo pamoja na kituo maalum cha kukuza vipaji vya michezo.

Wasaidizi wa Manji walikabidhi eneo hilo kwa Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa klabu hiyo mama Fatma Karume katika hafla fupi ambayo pia ilihudhuriwa na Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba.

Wasaidizi wa Manji walikabidhi eneo hilo jana mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na maofisa wa serikali ya Kigamboni.

Mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa Yanga, Fatma Karume ndiye aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu ambapo pia walikuwepo Dk Jabir Katundu, ambaye ni mjumbe wa baraza la wadhamini, mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Samuel Lukumay na Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit.

Manji amekabidhi eneo hilo ikiwa ana hesabu kadhaa zilizosalia kabla hajakabidhiwa timu baada ya mechi ya keshokutwa.


Baada ya kukabidhiwa eneo hilo, wadhamini wa klabu hiyo wanatarajia kulitambulisha rasmi kwa wanachama wao wiki ijayo. Eneo hilo lina ekari 715 ikiwa ni ukubwa zaidi ya eneo lililojenga Uwanja wa Uhuru.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com