Wednesday, November 23, 2016

Manchester United yamtamani Nyota wa Genk, mwenyewe awatahadharisha


Imeripotiwa kuwa Manchester United imetuma watu wake kwa ajili ya kumfuatilia winga chipukizi wa Genk ya Ubelgiji, Leon Bailey ili kumsajili baada ya msimu wa 2016/2017 kumalizika mwakani.
Inasemekana kuwa Man United inavutiwa na uwezo wa winga huyo mwenye miaka 19 na ipo tayari kumsajili ili kujiunga na kikosi cha klabu hiyo kinachonolewa na Mreno, Jose Mourinho.

Akizungumza kuhusu Man United kutaka kumsajili, Bailey alisema ana ndoto za kucheza Ligi Kuu ya Uingereza lakini kama Manchester United itashindwa kumthibitishia namba katika kikosi cha kwanza basi hatajiunga.


“Ninandoto za kucheza Ligi Kuu ya Uingereza, lakini kama Man United itanipangia dakika za kucheza, nitabaki Genk,” alisema Bailey.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com