Wednesday, November 23, 2016


WACHEZAJI wa Zesco United, kiungo Misheck Chaila na mshambuliaji Jesse Were wamesema kwamba hawajazungumza na Yanga SC juu ya mpango wa kumfuata kocha wao, George Lwandamina aliyetangulia kwa mabingwa hao wa Tanzania.


Tovuti ya Supersport imeandika kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya na kiungo wa Zambia wameripotiwa kuwa mbioni kujiunga na vigogo wa Tanzania katika dirisha hili la majira ya baridi kumfuata Lwandamina.

Were, ambaye amefunga mabao 15 katika msimu wake wa kwanza wa Zesco, kufuatia kujiunga na wababe hao wa Zambia kutoka Tusker ya kwao, Kenya Januari, amesema yeye 'bado yupo yupo' sana Zesco.

"Yote nayoweza kuzungumza kuhusu sakata la Yanga ni kwamba hawajazungumza na mimi. Kumekuwa na tetesi juu ya hili ndiyo, na nimesoma juu ya hili,” alisema Were.

Pamoja na hayo, Were amesema kwamba mpira upo miguuni mwa Zesco, kukubali au kukataa ofa ya Yanga ikitokea wakatuma maombi ya huduma zake.

"Lakini kwa sasa mimi ni mchezaji wa Zesco, nina mkataba, nina furaha, fikra zangu zipo kwenye mechi zilizosalia na nipo tayari kuwa hapa hadi nimmalize mkataba wangu mwishoni mwa msimu wa 2017,” alisema Were.

Kwa upende wake, Chaila amekanusha pia kufanya mazongumzo na Yanga au Lwandamina jus ya kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania.

“Hakuna hate momma aliyezungumza na mimi au klabu. Zote ni tetesi tu,” alisema Chaila. “Hakika sijazungumza naye (Lwandamina) tangu aondoke, lakini namuheshimu kama mzazi wangu,".”

Jesse Were amesema Zesco ndiyo wenye maamuzi iwapo Yanga watatuma maombi ya kutaka huduma zake


0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com