Thursday, November 17, 2016

SERIKALI YA TANZANIA YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU ICC



Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa nchi wanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, kuendelea kuunga mkono uwepo wa chombo hicho wakati huu ambapo baadhi ya nchi zinaendelea kujitoa.

Akizungumza huko The Hague, Uholanzi kwenye mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa Roma ulionzisha ICC, Zeid amesema kujitoa kwa baadhi ya nchi kunaonekana kuwa na lengo la kulinda viongozi wao dhidi ya mashtaka.

Amesema anasikitishwa na hali ilivyo kwani nchi za Afrika zimekuwa msingi wa mahakama hiyo, lakini anatiwa moyo kuwa Botswana, Cote d'Ivoire, Nigeria, Malawi, Senegal, Tanzania, Zambia na Sierra Leone zimesema zitaendelea kuwa wanachama.

Zeid ametoa kauli hiyo wakati huu ambapo yaelezwa Urusi ina mpango wa kujitoa, wakati nchi tatu za Afrika; Burundi, Afrika Kusini na Gambia tayari zilishatangaza kujitoa

 Hii leo imeelezwa kuwa baadhi ya nchi zimesema zitaendelea kuwepo ndani ya chombo hicho cha haki, nazo ni Botswana, Cote d'Ivoire, Nigeria, Malawi, Senegal, Tanzania, Zambia na Sierra Leone.
Kamishna wa haki za binadamu Zeid Ra'ad al Hussein amepongeza hatua hiyo akisema chonde chonde jamani msitoke!

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com