Wednesday, January 18, 2017

Okwi avunja mkataba na Sonderjyske Fodbold, Kurejea Simba?


Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda,  Emmanuel Okwi ameachana rasmi na klabu ya  Sonderjyske Fodbold ya Denmark kwa makubaliano ya pande zote kuamua kusitisha mkataba.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Danish Superliga Jorgen Haysen uamuzi huo umefikiwa baada ya Okwi kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.
“Okwi hakuwa anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi chetu, na matumaini ya kupata nafasi yamekuwa ya chini sana. Matokeo yake tumekubaliana kububja mkataba, tunamtakia kila la kheri huko mbeleni.’
Klabu hiyo ilimsaini Okwi mnamo July 2015 kwa mkataba wa miaka 5 akitokea klabu ya Simba SC ya Tanzania bara.
Katika dirisha la usajili lililopita kulikuwa na taarifa kwamba mchezaji huyo alikuwa njiani kurejea Msimbazi, hata hivyo ilishindikana kutokana na ada ya usajili waliyokuwa wanataka Sonderjyske Fodbold. 

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com