Friday, November 25, 2016

LWANDAMINA AKABIDHIWA TIMU RASMI LEO NAKUSMA HAYA..


Geroge Lwandamina ametambulishwa rasmi kuwa kocha mpya wa Yanga SC akirithi nafasi ya kocha wa zamani wa klabu hiyo Hans van der Pluijm ambaye amepewa majukumu mapya ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi ndani ya klabu hiyo inayotetea ubingwa wake wa VPL ilioutwaa msimu uliopita.
|"amesema kwamba atafanya kazi na Maofisa aliowakuta benchi la Ufundi na hataleta mtu mpya.Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam wakati wa utambulisho wa wakuu wapya wa Idara ya Ufundi, Lwandamina alisema kwamba hana mpango wa kubadilisha chochote kwenye benchi la Ufundi.Na kuhusu kuongeza wachezaji, Lwandamina amesema kwamba ameiona Yanga katika mechi yake ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikishinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting na amegundua "ni timu nzuri ambayo haihitaji mchezaji mpya.
Lwandamina amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomuweka Jangwani.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amewatambulisha wawili hao ndani ya makao makuu ya klabu ya Yanga na kumkabidhi Lwandamina jezi ya Yanga ikiwa ni ishara ya utambulisho na kumkaribisha ndani ya klabu.

Pluijm pia ametangazwa rasmi kuchukua majukumu mapya ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi akiachana na masuala ya ukocha ndani ya klabu hiyo aliyoipa mafanikio makubwa ikiwa chini yake kama kocha mkuu.

Lwandamina amekabidhiwa klabu ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara pointi mbili nyuma ya vinara wa ligi Simba ambao wanapointi 35 baada ya mzunguko wa kwanza kumalizika.

Kocha huyo (Lwandamina) aliifikisha Zesco United hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika msimu uliomalizika hivi karibuni, atakuwa na kibarua kuhakikisha anatetea taji la VPL, Azam Sports Federationa Cup (FA Cup) pamoja na kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa ambapo msimu uliopita ilifika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika chini ya Pluijm.

Kocha huyo mpya wa yanga akitoa sifa kemukemu:

Alimsifu mtangulizi wake, Pluijm kwamba amefanya kazi nzuri na akasema atafuata nyayo zake na atashirikiana naye bega kwa bega kuhakikisha Yanga inapata mafanikio zaidi.
Lwandamina amekana madai kwamba amependekeza wachezaji wawili aliokuwa nao Zesco United ya kwao, Zambia kiungo Misheck Chaila na mshambuliaji Mkenya Jesse Were wasajiliwe pia. 
Baada ya kuiongoza Yanga katika jumla ya mechi 128 kwenye awamu mbili, akishinda 80, sare 25 na kufungwa 23, Pluijm aliyetua Jangwani mwaka 2014 anampisha Lwandamina.
Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 110 za tangu mwaka jana, alishinda 69, sare 19 na kufungwa 21.
Na anahama nafasi baada ya msimu mzuri uliopita, akibeba mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC).
Pluijm pia aliiwezesha Yanga kufika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika (Kombe la Shirikisho) kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 na mara ya pili kihistoria. Yanga ilifika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu baada ya mwaka 1998 kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
Na kwa mafanikio hayo, haikuwa ajabu Pluijm akishinda tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu uliopita. 
Benchi jipya la Ufundi Yanga sasa linakuwa chini ya Pluijm kama Mkurugenzi, Lwandamina Kocha Mkuu, Juma Mwambusi Kocha Msaidizi, Juma Pondamali Kocha wa makipa, Hafidh Saleh Meneja, Daktari Edward Bavu, Jacob Onyango Mchua Misiliu na Mtunza Vifaa Mohamed Omar ‘Mpogolo’.



0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com