Wednesday, May 3, 2017

Mkwasa asema aina mpango wa kuwatema wachezaji Yanga


Bonifasi Mkwasa Katibu Mkuu wa Yanga

Katibu Mkuu wa Yanga SC,  Charles Boniface Mkwasa amekanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba wana nia ya kuwaacha baadhi ya wachezaji wake na kusema hizo taarifa na uzushi mkubwa ndani ya klabu yao.


Mkwasa amebainisha hayo kupitia taarifa yake aliyoitoa asubuhi ya leo baada ya kuenea kwa taarifa kutoka baadhi ya vituo vya Radio na 'social network' zikidai klabu hiyo inataka kuwabwaga baadhi ya wachezaji wake kutokana na kufanya vibaya katika Ligi.
"Taarifa hizo ni za uongo na uzushi mkubwa, uongozi upo bega kwa bega na wachezaji wote 27 na benchi la ufundi. Hatujakaa kulijadili hilo wala kulifikiria bali tupo makini kutetea ubingwa wetu wa ligi kuu". Alisema Mkwasa
Aidha, Mkwasa alisisitiza kwamba Kocha Mkuu, George Lwandamina ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho juu ya huduma ya wachezaji ndani ya klabu hiyo na wala siyo kiongozi mwingine yoyote
"Kocha Mkuu George Lwandamina hajatoa taarifa yoyote ya kumwacha mchezaji gani au yupi wa kumuongezea mkataba,  zaidi ya kila siku kuukazia uongozi kuboresha masilahi ya wachezaji kwa sababu kama kocha mkuu anajivunia na kujali kazi ya vijana wake". 

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com