Wednesday, May 3, 2017

Himid aka Niinja kwenda Ulaya kutafuta maisha ya soka la kulipwa


himid mao akiwa Denmark ndani ya uwanja wa timu ya Randers FC

Kiungo wa Azam FC  na timu ya taifa ya Tanzania Himid Mao ameondoka nchini jioni ya leo Mei 1, 2017 kuelekea Denmark kwa ajili ya majaribio ya kutafuta kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Himid anakwenda kwenye klabu ya Randers FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo ligi inayojulikana kwa jina la Superliga.

Kiungo huyo ameonesha kiwango cha juu katika msimu huu kuanzia kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara, kombe la Azam Sports Federation Cup, michuano ya kimataifa pamoja na mechi za timu ya taifa.shaffihdauda.co.tz ilizungumza na Himid Mao muda mfupi kabla hajaondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Nyerere.
“Naenda kwenye klabu ya Randers FC ya nchini Denmark kwa ajili ya majaribio kwa muda wa siku 15, kama mchezaji najiamini naweza kufanya lolote sehemu yoyote, mambo mengine ya mbeleanajua Mungu,” amesema Himid muda mfupi kabla ya kuondoka ardhi ya Bongo.

“Mimi wajibu wangu ni kujitolea kadiri niwezavyo na kuwashawishi hao kwa uwezo wangu wote patakapobakia ni kazi ya Mungu.”
“Kila kitu kipo kama kilivyopangwa, klabu yangu inajua, wakala anajua kwa hiyo kila kitu kipo wazi utakapofika wakati wa klabu kutangaza chochote watafanya hivyo.”

“Kwa sasa naangalia hiki kilichopo mbele halafu baadae tutajua nini kitakachofuata.”

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com