Wednesday, May 3, 2017

Viongozi kutoka Ukanda wa CECAFA wakubaliana kuimarisha soka



Marais kutoka mataifa yanayounda Baraza la soka Afrika Mashariki CECAFA, walikutana jijini Kampala nchini Uganda siku ya Jumatano kuzungumzia namna ya kuboresha mchezo wa soka katika ukanda huo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na marais saba wakiongozwa na mwenyeji wao Moses Magogo, Vincent Nzamwita kutoka Rwanda, Jamal Malinzi (Tanzania), Juneidi Tilmo (Ethiopia), Nicolas Mwendwa (Kenya) na Ndikuniyo Reverien (Burundi).
Ravia Faina rais wa Shirikisho la soka kutoka kisiwa cha Zanzibar kilichopewa uanachama wa CAF hivi karibuni, pia alikuwepo.
Mambo saba yaliyoafikiwa katika mkutano huo ni pamoja na:-
1 – Kuibadilisha Katiba ya CECAFA.
2 – Kuandaa mkutano mkuu wa CECAFA haraka iwezekanavyo.
3 – Kuhakikisha kuwa CECAFA inapata Makao makuu ya kudumu.
4 – Kuimarisha michuano ya vijana wasiozidi miaka 15, 17 na 20 kwa wavulana na wasichana pamoja na kuboresha soka la ufukweni.
5 – Kuimarisha hali ya waamuzi uwanjani, makocha, uongozi lakini pia hali ya matibabu kwa wachezaji.
6 – Kuimarisha mawasiliano na kuitangaza CECAFA.
7 – CECAFA kuomba nafasi ya kuandaa fainali ya mataifa bingwa barani Afrika katika siku zijazo.
8 –CECAFA kuwakilishwa ipasavyo katika Kamati kuu ya CAF.
9 –Kuja na mbinu za kuandika mapendekezo kwa Shirikisho la soka duniani FIFA ili kusaidia kuinua soka la vijana, wanawake na lile la ufukweni.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com