Monday, February 6, 2017

Mtanzania anayecheza soka PSG ya Ufaransa




Mtanzania Haytham Saduun ameeleza safari yake ya soka ilivyokuwa kutoka Bongo hadi kufika kwenye academy ya PSG ya Ufaransa moja kati ya vilabu vikubwa barani Ulaya.
Haytham ambaye kwa sasa anamiaka 18, safari yake ya soka imeanzia katika timu ya vijana ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro ambapo alikuwa anakipiga kabla ya kwenda Uarabuni kwa matembezi kisha kutumia fursa hiyo kusonga mbele zaidi.
Kijana huyo anaetokea maeneo ya Temeke-Mwisho (Kitomondo au Wailes) anasema alipata safasi ya matembezi kwenda Oman ambapo wakati yupo huko alipata fursa ya kucheza kwenye academy ya Muscat akaonesha uwezo wakamuhitaji na kumpa muda zaidi.


Safari ilivyoanza
“Nilipata nafasi ya kwenda Urabuni (Oman) nikapata nafasi ya kucheza academy ya Muscat baada ya kufanyiwa trial kwa siku tatu. Kulikuwa na safari ya kwenda Dubai kwa ajili ya mashindano ya Dubai Super Cup, tulicheza mashindano yale na kufanikiwa kuchukua ubingwa huku mimi nikifanikiwa kufunga magoli matatu katika michuno hiyo na kuonesha kiwango kizuri,”-Haytham.


Dili la PSG linaibuka
Kulikuwa na ma-scout mbalimbali kutoka nchi za Ulaya, alikuwepo pia muwakilishi kutoka Ufaransa ambaye alinihitaji kwa sababu alianza kunifatilia tangu nikiwa academy (Muscat, Oman).
Alinifanyia mipango ya kunipeleka Paris St Germain baada ya kila kitu kukamilika tukaenda pamoja na wenzangu wengine kwa ujumla tulikuwa watu sita. Tukafanya trial kwa muda wa siku tano na bahati nzuri nikafanikiwa kufuzu mimi pekeangu.

Imepata sponsorship ya kuingia professional kwa hiyo mwaka huu kama Mungu akipenda naweza nikafika hapo kutokana na mipango inayofanyika sasa hivi


Vipi kuhusu kuitumikia Tanzania?
Nilipata nafasi ya kubadilisha uraia lakini uongozi wangu ukakataa kwa sababu tuna kauli yetu moja inaitwa ‘Tanzania Kwanza’. Mimi nipo tayari kujitolea kuitumikia nchi yang na kuitangaza hata kama ningekuwa na mguu mmoja nikiitwa timu ya taifa nitakuwa tayari.

Ushauri kwa vijana wa kibongo
Nimepitia mambo mengi magumu sana katika harakati zangu, lakini kumuweka Mungu mbele ni muhimu sana. Hapa nyumbani ushirikina umewekwa mbele sana lakini uchawi kwenye mpira ni mazoezi, jitihada binafsi na nia.

Hakuna kinachoshindikana chini ya jua, nitajitahidi na kuongeza nguvu zaidi na kufanya kila kinachowezekana huku nikiweka mbele malengo yangu ya kufika sehemu ninayotaka, natamani kuwa mchezaji wa kwanza kucheza ligi kuu ya Ufaransa.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com