Sunday, May 14, 2017

Hiki Ndicho Alichosema MO kwa simba
Baada ya  simba na SportPesa Tanzania rasmi  kutangza udhamini wake wa miaka mitano kwa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, wenye thamani ya Sh. Bilioni 4.96.

MO kawaandikia Simba ‘demand note’ kwa kua wamekiuka makubaliano yao kwamba, atoe pesa kama makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba inabidi wakae meza moja viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba, lakini viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya.

Simba ilishaanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokua ombi la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama wakibaki na hasilimia 49.
Adi kufikia leo akuna majibu yoyote yaliotoka simba na hiki ndicho alichokiandika Mo kwenye hukurasa wake wa instagram"Inasikitisha kuwa uongozi wa Klabu ya Simba umesaini mkataba wa udhamini wa muda mrefu bila kunishirikisha. Kwa muda mrefu nimeweka nguvu zangu kwenye klabu."


0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com