Taarifa Kuhusu Hali ya Saimoni Msuva
Nyota wa timu ya yanga Msuva alipata jeraa wakati wa mpambano wao zidi ya mbeya city uluiofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam huko yanga kuibuka na ushindi mnono wa ngili mbili kwa moja ,Yanga ndio walioanza kuongoza kwa ngoli moja lilo fungwa na Msuva kupelekea kuchanika juu ya jicho lake la kushoto
ambapo ameshonwa nyuzi nne baada ya kugongana na mchezaji wa Mbeya city wakati
akifunga goli lake la 14 kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Ushindi
huo unawafanya mabingwa hao watetezi watimize pointi 65 baada ya
kucheza mechi 28 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu. Simba inaangukia nafasi
ya pili kwa pointi zake 65 za mechi 29, ikizidiwa wastani wa mabao.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Andrew Shamba wa Pwani, aliyesaidiwa na Joseph Pombe wa Shinyanga na Haji Mwalukuta wa Tanga, dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika Yanga ikiwa inaongoza 1-0.
Hata
hivyo, Yanga wakafanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na
mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa dakika ya 64 akimalizia mpira wa
adhabu wa Juma Abdul.
Mbeya City ilijitahidi kujaribu kusawazisha bao hilo, lakini tayari wapinzani wao, Yanga walikuwa wamekwishaanza kucheza kwa kujihami zaidi na kushambulia kwa kushitukiza.
Mrisho Ngassa aliingia kipindi cha pili upande wa Mbeya City, lakini hakuwa na madhara kwa timu ya timu yake ya zamani zaidi tu ya kusisimua mashabiki kwa uchezaji wake mzuri.
Kikosi cha Yanga; Benno Kakolanya, Hassan Kessy/Emmanuel Martin dk, Mwinyi
Hajji Mngwali, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’/Kevin Yondan
dk67, Thabani Kamusoko, Simon Msuva/Juma Abdul dk12, Haruna Niyonzima,
Amisi Tambwe, Obrey Chirwa na Geoffrey Mwashiuya.
Mbeya City; Owen Chaima, Haruna Shamte, Hassan Mwasapili, Tumba Lui, Sankani Mkandawile, Kenny Ally, Ditram Nchimbi, Majaliwa Shaaban, Zahor Pazi/Bryson Raphael dk46, Raphael Daudi na Rajab Isihaka/Mrisho Ngassa dk58.
0 comments:
Post a Comment