Wednesday, November 16, 2016

SERIKALI IMEPANIA KUBADILISHA UONGOZI WOTE WA ATCL


Tanzania inapanga kuufanyia mabadiliko uongozi wa Shirika lake la ndege
Tanzania imesema inapanga kuufanyia mabadiliko uongozi wa shirika lake la ndege ili libaki na wafanyakazi bora, na kuboresha utendaji wa shirika hilo.

Waziri wa ujenzi, usafirishaji na mawasiliano wa Tanzania Prof Makame Mbarawa, amesema ili shirika hilo liweze kuhimili ushindani wa kikanda linatakiwa kuboresha utendaji wake.

Amesema serikali ya awamu ya tano ina nia thabiti ya kuboresha shirika hilo na kuwa moja ya mashirika mazuri kwenye eneo la Afrika Mashariki ndani ya miaka mitano. Kwanza ameupa uongozi wa juu wa shirika hilo muda wa mwezi mmoja kufanya mabadiliko ili kubaki na wafanyakazi wenye uwezo.

Hivi karibuni serikali ya Tanzania iliagiza ndege mbili za abiria, na imepanga kuagiza ndege mbili zaidi, na kuhakikisha kuwa kabla ya mwaka 2018 inakuwa na ndege saba.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com