JPM aagiza kufutwa kwa utitiri wa kodi
Ikiwa Tanzania Inataraji Mpaka ifikapo waka 2020 iwekweyne uchumi wakati hivi leo Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wakuu wa Mikoa,Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuondoa utitiri wa kodi uliopo kwenye Mazao ili wakulima waweze kunufaika kutokana na kujiongezea kipato.
Agizo
hilo alimetolewa leo wakati akihutubia wakazi wa Wilaya ya Bukoba na
watanzania kwa ujumla akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani
Kagera.
“Nawaagiza Wakuu wa Mikoa,Wilaya pamoja
na Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia upya Kodi zilizopo katika bidhaa
mbalimbali kama Kahawa na Pamba, hakikisheni mnaondoa utitiri huu wa
Kodi ili wafanyabiashara hawa wafaidike na mazao yao,” Alisema Rais
Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amewaahidi
watanzania kuwa atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana bila kujali
itikadi, dini na makabila ili kuhakikisha nchi inasonga mbele katika
nyanja zote za kimaendeleo.
Akizungumzia maendeleo ya michango
mbalimbali kwa ajili ya wathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera
Rais Magufuli amesema kuwa mpaka sasa simenti iliyochangwa ni zaidi ya
tani 30,600 na mabati zaidi ya elfu 31,000 ambapo wananchi wameshaanza
kupewa na kujengea.
Amewahimiza wananchi walioathirika na
tetemeko la Ardhi kutotegemea Serikali kuwafanyia kila kitu na badala
yake waanze kujenga na watumie msimu huu wa mvua kulima ili kujipatia
chakula.
Pia Rais Magufuli amewashukuru na
kuwapongeza wahisani waliochangia Maafa ya Kagera na kuwataka kuendelea
na moyo huo katika kulijenga Taifa letu.
0 comments:
Post a Comment