RC Shinyanga azuiwa kuingia mgodini
Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack, umezuiwa kuingia katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini, TMAA.
Maofisa
wa TMAA waliondoka mara baada ya ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa
dhahabu kukabidhiwa kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli hapo jana ikulu
jijini Dar es sallaam.
Bi. Zainabu amesema ameagiza Jeshi la
Polisi kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha
hakuna mtu anayetoka wala kuingia
Mapema leo Mkuu huyo wa Mkoa alitembelea
mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia
kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.
Katika mgodi wa Buzwagi, Bi. Zainab na
msafara wake waliruhusiwa kuingia na kushuhudia shughuli za uchimbaji
zikiwa zimesitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara
baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa
watendaji wakuu wa wakala hiyo.
0 comments:
Post a Comment