UNESCO wajenga kituo cha kumbukumbu za jamii ya KIMASAI
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) |
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO, kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya –EU- wamejenga kituo cha utamaduni kitakachotumika kutunza kumbukumbu muhimu za jamii ya kimasai na kutoa elimu za kitamaduni kwa njia ya kieletroniki katika wilaya ya NGORONGORO mkoani ARUSHA.
Mwakilishi wa UNESCO nchini, ANNA CONSTANTINE, amesema kituo hicho kitasaidia kutoa elimu mbali mbali hasa kuhusu namna ya kuhifadhi tamaduni
Kwa upande wake Mwakilishi toka Umoja wa Ulaya- EU-OLIVIER COUPLEX, amesema makubaliano yakuanza ujenzi wa mradi huo wa kituo cha utamaduni ulifikiwa mwaka 2012 baina ya serikali ya TANZANIA na Umoja wa Ulaya EU.
Mkuu wa mkoa wa ARUSHA, MRISHO GAMBO, amelishukuru shirika la UNESCO pamoja na Umoja wa ulaya EU kwa jitihada mbali mbali za kuleta maendeleo nchini na pia amesema kituo hicho kitasaidia kutunza kumbukumbu muhimu kuhusu tamaduni za maasai kutokana na jamii hiyo kuwa na tamaduni nyingi ambazo zimekuwa kivutio kikubwa ndani na nje ya nchi.

0 comments:
Post a Comment