China yafungua Milango kwa vijana wa kitanzania
Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustino Mahiga amesema China imekubali kutoa fursa za masomo nchini mwao kwa vijana wa Tanzania ambao ndiyo watapewa kipaombele cha ajira katika viwanda vitakavyowekezwa na nchi hiyo hapa nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4;00 asubuhi hadi saa 11 jioni na yanatarajiwa kumalizika kesho tarehe 22 Januari 2017.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo
katika sherehe za maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaofahamika kama
'Jogoo', Balozi Mahiga amesema ni wakati sasa kwa watanzania
kuchangamkia fursa hiyo ya masomo ili kupata ajira nyingi za watanzania.
Kwa upande wake waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji akizungumza katika sherehe hizo Charles Mwijage
amesema kuna miradi mingi ya uwekezaji ya China ambayo itawekezwa hapa
nchini ikiwemo bandari na viwanda vitakavyoshughulika na teknolojia
mbalimbali
0 comments:
Post a Comment