Tuesday, November 29, 2016

UTAFITI WA KWANZA WA CHANJO YA HIV YA ANZA KUSINI MWA AFRICA


Utafiti kuhusu ufanisi wa chanjo ya kwanza ya VVU waaanza huko Afrika Kusini! Je, una imani chanjo hiyo itatokomeza UKIMWI?


Taasisi ya Afya ya Marekani imesema, utafiti kuhusu ufanisi wa chanjo ya kwanza ya VVU utakaodumu kwa miaka saba umeanza nchini Afrika Kusini, ili kujaribu kama chanjo hiyo inaweza kutoa kinga yenye ufanisi dhidi ya virusi vya UKIMWI. Utafiti huo unalenga kuwashirikisha wanaume na wanawake 5,400 wenye umri wa miaka 18 hadi 35, na kuwa majaribio makubwa zaidi ya chanjo ya VVU nchini Afrika Kusini, ambako zaidi ya watu elfu 1 wanaambukizwa virusi hivyo kila siku.

Tumepata maendeleo mengi katika mapambano dhidi ya UKMWI, lakini bado hatujafanikiwa kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo. 

Je, Una imani kuwa sisi binadamu tunaushinda ugonjwa huo? Unadhani itachukua miaka mingapi kupata ushindi wa mwisho katika mapambano hayo dhidi ya UKIMWI?

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com