Mbunge Chadema atupwa jela miezi sita
Mahakama ya wilaya ya Kilombero imemuhukumu kifungo cha miezi sita jela Mbunge Wa jimbo la Kilombero Peter Lijualikali (30) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero
Mwendesha mashtaka inspekta Wa Polisi
Dotto Ngimbwa aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa, akiwa mshtakiwa namba
moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo Machi
mosi mwaka 2016 saa 4 asubuhi Kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika
eneo la Kibaoni ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Ngimbwa alisema washtakiwa hao kwa
pamoja walifanya fujo kinyume na kifungu namba 89 kifungu kidogo cha
kwanza B, cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo
mwaka 2002, ambapo washtakiwa walikana mashtaka na hivyo kufanya kesi
kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na upande wa mashtaka
ukathibitisha shtaka bila kuacha shaka.
Hakimu mkazi katika mahakama ya wilaya
ya Kilombero Timothy Lyon alisema mahakama imewatia hatiani kwa kosa
hilo na kwa kuwa mshtakiwa Wa kwanza ni Mbunge ambaye alikuwa na kesi
tatu huko nyuma na kutiwa hatiani amehukumuwa jela miezi sita.
Moja kati ya matukio ya vurugu
yaliyomuhusisha mbunge huyo, na hapa ilikuwa ni katika kikao cha
uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri
Hata hivyo mahakama hiyo imeona kwa kuwa
mshtakiwa wa pili Stephano Mgata (35), hii ni Mara yake ya kwanza
amehukumiwa kifungo cha miezi sita nje ambapo ndani ya kipindi hicho cha
miezi sita hatotakiwa kutenda kosa lolote la jinai.
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya
kawaida hali katika mahakama hiyo ilikuwa tulivu tofauti na kesi
nyingine dhidi ya Mbunge Lijualikali, ambapo wafuasi wachache
wanaodhaniwa kuwa ni wa Chadema ndiyo walijitokeza na baada ya hukumu
kutolewa Mbunge huyo alipelekwa haraka gerezani kwenda kuanza kutumikia
kifungo chake
Kutokana na jambo hili mwanasiasa Julius
Mtatiro anasema kuwa licha ya Lijualikali kufungwa jela lakini hali
hiyo haiwezi kupoteza ubunge wake na kusema kama akikata rufaa huenda
akapata haki.
"Hawezi kupoteza ubunge kwa kifungo
hicho na kama akikata rufaa anaweza kupata haki, Kumfunga Lijuakali kwa
sababu alihoji na kupinga kunyimwa haki yake ni kuzalisha Lijualikali
wengi zaidi" alisema Julius Mtatiro
0 comments:
Post a Comment