Thursday, January 12, 2017

Wateule' wamrudisha Solo Thang




Rapa mkongwe Bongo Jay Moe amesema ujio wa Solo Thang bongo ni mzuri kwani amekuja kufanya kazi zake mwenyewe kama Solo Thang lakini pia wao kama Wateule hawatakubali kuona Solo Thang ameondoka Bongo bila kufanya kazi ya pamoja.

Akiongea kwenye kipindi cha eNEWZ Jay Moe amesema wanataka wao wenyewe waweze kujisimamisha kwenye ushindani wa muziki wa sasa na kuona kila mmoja kati yao anakuja na project yake na kusimama kivyake kisha watafanya project za kundi kama Wateule.

"Usishangae kesho, kesho kutwa Solo Thang amekuja na project na msanii mwingine wa kizazi hiki cha sasa, lakini ukiacha hapo hatuwezi kumruhusu Solo Thang aondoke bila ya kuwa na wimbo wowote ule wa Wateule, ikiwezekana moja mbili au tatu kabisaa kwa sababu saizi ni rahisi studio tunazo nyingi, beats tunazo kibao tunataka sisi wenyewe tuweze kujisimamisha kwenye competition inayoendelea kwenye soko la muziki sasa hivi" alisema Jay Moe 

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com