Serengeti Yatoshana Nguvu na Afrika Kusini kwao
Afrika Kusini iliyopania kupata ushindi kwao, kwenye Dimba la Dobsonville, Soweto jijini Johannesburg, imeshindwa kutamba mbele ya vijana Watanzani Serengeti Boys baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Luke Gareth kwa penalti baada ya mchezaji mmoja wa Serengeti Boys kumfanyia madhambi ndani ya 18 Gareth katika dakika ya 65. Lakini dakika ya 70, Ally Msengi aliisawazishia Serengeti Boys bao pia kwa penalti iliyotokana na Beki, Sechaba Makoena kushika mpira ndani ya eneo la hatari. Mwamuzi wa mchezo alikuwa William Koto kutoka Lesotho.
Kwa matokeo ayo nimwanzo mzuri kwa upande wa timu ya serengeti boys ambayo italazimika kusubi duru ya pili itakayo chezwa hapa Tanzania.
Mchezo wa marudiano utachezwa Agosti 21, kwenye uwanja wa Azam Compolex, Chamazi, Dar es Salaam. Endapo Serengeti Boys itafanikiwa kuitupa nje ya mashindano timu ya vijana ya Afrika Kusini, itatinga hatua ya mwisho ya mchujo kabla ya kufuzu kwa ajili ya fainali hizo.
0 comments:
Post a Comment