Sasa Imetosha Kuwa na dada na kaka poa Kinondoni
Licha
ya Serikali kuanzisha vita dhidi ya biashara haramu ya uuzaji mwili,
Wilaya ya Kinondoni inakabiliwa na ongezeko la biashara haramu ya ngono
kwa muda mrefu ambapo eneo la Tandale linatajwa kukithiri vibanda vingi
vya dada na kaka poa.
Wakuu
wa wilaya wengi wamepita katika wilaya ya Kinondoni pasipo kutokomeza
changamoto hiyo. Lakini Mkuu wa sasa wa Wilaya hiyo Mh. Ally Hapi
amejidhatiti kuuvunja mwiko huo. Hivi karibuni Hapi alitaja mikakati ya
kutokomeza mtandao wa biashara hiyo.
Alisema
atahakikisha anavunja vibanda vyote vinavyotumiwa na dada pamoja na
Kala poa , vilevile watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hapi
alisema amepokea idadi ya vibanda vinavyotumiwa na dada poa na kwamba
mpango wake ni kuvifunga kisha kutafuta wawekezaji ili Wamiliki wa
vibanda hivyo walipwe fidia na kupisha ujenzi wa vitega uchumi.
“Niliwaagiza
watendaji wa kata kuniletea idadi ya madanguro, nimeshajua mahali
yalipo madanguro hayo, na kwamba nitakwenda kuchukua hatua ya kufunga
madanguro pamoja na kuwapeleka dada poa mahakamani,” alisema. Alisema
hatawachukulia hatua za kisheria dada/kaka poa pekee, bali hata wamiliki
wa baa zitakazowahifadhi watu hao watachukuliwa hatua.
“Hatutashughulika na dada poa pekee bali hata Wamiliki wa nyumba na au baa watachukukiwa hatua. Hilo likitekelezwa
Kila mtu atatimiza wajibu wake,
nimegundua wamiliki wengi wa madanguro hawapo hapa na idadi ya madanguro
katika eneo la Tandale pekee kuna vibanda 58.” alisema.
Alisema
utekelezaji wa ubomoaji nyumba umeshaanza kujadiliwa na kwamba
wanasubiriwa wawekezaji ili wapewe fursa za kujenga maduka na vitega
uchumi.
“Tunataka wenye fedha zao waje wawekeze ili tuwalipe fidia wenye nyumba, zibomolewe,” alisema na kuongeza.
“Huu mfupa uliwashinda watangulizi wangu lakini mimi nitautafuna.”
Kuhusu
baa zinazokiuka sheria, alisema atawaondoa watendaji wa kata waliokaa
muda mrefu kwa sababu wengi wao ndiyo chanzo cha ukiukwaji wa sheria.
“Watendaji
waliokaa muda mrefu waondolewe sababu tumegundua hushirikiana na wenye
baa kupiga kelele, wanachukua fedha zao na kuwaacha kupiga kelele usiku
wa manane kinyume cha tarabibu,”
0 comments:
Post a Comment