Monday, August 22, 2016

Afrika Mashariki yatakiwa kuboresha sheria kwenye sekta ya uchimbaji madini





 Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki EADB imezitaka nchi za kanda hiyo kuboresha sheria kwenye sekta ya uchimbaji madini ili kuhakikisha rasilimali zinapangwa kwa usawa.
Akiongea kwenye semina ya kikanda ya majaji kutoka nchi za Afrika Mashariki iliyomalizika jana Nairobi, Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Vivienne Yeda, amesema ugunduzi na uchuguzi unaoendelea wa madini katika kanda hiyo umeongeza matumaini ya kuongeza utajiri, kupunguza nakisi ya bajeti na kuboresha maisha ya watu wa nchi hizo. Amesisitiza kuwa mafao lazima yaende kwenye jamii za nchi husika, kwa njia za mirahaba, kodi, mgao, fursa za biashara, kazi za kitaalamu na ajira kwa wafanyakazi wenye ujuzi.
Semina hiyo iliyoandaliwa na EADB, imewalenga majaji wa Afrika mashariki wanaohusika na kazi ya usuluhishaji na kutatua migogoro kwenye sekta ya madini.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com