Tanzania kujitengeneza ndege aina ya helikopta Kwa Mara Ya Kwanza
Raia nchini Tanzania wameamkia habari za kushangaza kwamba taifa hilo linaunda ndege.
Gazeti
la Tanzania la Daily News limeripoti kwamba ndege hiyo aina ya
helikopta inakaribia kukamilika na kwamba habari hiyo imekuwa ikisambaa
barani Afrika kwa kasi.Gazeti la Zambia, Observer linasema kuwa lengo la ndege hiyo itayokuwa ikibeba watu kwa bei rahisi itakabiliana na matatizo ya uchukuzi nchini humo.
Huku gazeti la Cameroon, Concord likisema kuwa mradi huo ni wa kihistoria linaongezea kuwa lengo lake ni kutengeza ndege 20 kwa mwaka.
Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu wawili inakaribia kukamilika katika chuo cha ufundi cha Teknolojia cha Arusha na itaanza kufanyiwa majaribio ya kuruka angani baada ya kuruhusiwa na mamlaka ya uchukuzi wa angani nchini Tanzania kulingana na Daily News.
WAZUNGU WAMTEMBELEA MTENGENEZAJI HELIKOPTA TUNDUMA
** Mkazi wa Tunduma, mkoani Songwe, Adam Kinyekile (34) ambaye alikuwa akitengeneza helikopta amepata mwaliko maalumu na wazungu kutoka Afrika Kusini kutembelea kiwanda chao cha kutengeneza chopa.
Kijana Kinyekile ambaye pia ni fundi magari alitumia ubunifu wake kuunda helikopta, kitu ambacho kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, George Mbijima akiwa mjini Tunduma alimtembelea kisha kuweka jiwe la msingi kwenye helikopta hiyo.
Hata hivyo baada ya taarifa za kijana huyo kurushwa kwenye vyombo vya
habari , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilipiga marufuku kwa
mtu yoyote kutojihusisha na utengenezaji au ubunifu wa ndege bila
kufuata taratibu.
Onyo hilo lilionekana kumlenga Kinyekile kwa kazi yake aliyokuwa akiifanya jambo ambalo lilimfanya asiweze kuendelea na maboresho ya helikopta yake licha ya kudai ilikuwa imebaki kuruka.
Onyo hilo lilionekana kumlenga Kinyekile kwa kazi yake aliyokuwa akiifanya jambo ambalo lilimfanya asiweze kuendelea na maboresho ya helikopta yake licha ya kudai ilikuwa imebaki kuruka.
0 comments:
Post a Comment