Wasimamizi wa kazi za Prince wamezikataa Dola milioni 40 za Jay Z
Rapper Jay
Z alituma barua ya maombi kwa uongozi wa legend wa muziki Marekani
marehemu Prince, na kuomba umiliki wa nyimbo zake ambazo mpaka kifo
chake alikuwa hajazitoa. Inasemekana Jay Z alitenga dola za kimarekani
milioni 40 kwa ajili ya kukamilisha deal hilo.
Baada ya
kuzungumza na uongozi wa Prince umekataa kusaini deal hilo na rapper
huyo, ukidai kuwa Jay Z alishawahi kuziachia albamu 15 za Prince kwenye
mtandao wake wa Tidal miezi michache tu baada ya Prince kufariki bila
kibali chochote, na wanaamini Jay Z aliingiza pesa ndefu hivyo kuna
uwezekano wa kumfungulia rapper huyo kesi ya madai.
Hata hivyo inasemekana uongozi unaosimamia
kazi za Prince unafahamu Jay Z alikubaliana na Prince kuwa atasimamia
albamu yake ya “HitNRun Phase One” ya mwaka 2015 lakini hakuna nyaraka
za mikataba zinazoonyesha malipo ya dolla 750,000 ambazo ndio zilipaswa
kulipwa ili kufunga mkataba.
0 comments:
Post a Comment