Hans van Pluijm amejiuzulu Yanga baada ya kusikia ujio wa kocha mpya
Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Hans van der Pluijm ameandika barua ya kujiuzulu kuifundisha klabu hiyo ya Jangwani.
Uamuzi wa Pluijm umekuja baada ya tetesi kuzangaa kwamba uongozi wa klabu hiyo unampango wa kubadili benchi la ufundi la klabu hiyo huku yeye kama kocha wa sasa akiwa hana taarifa rasmi kutoka kwa klabu.
“Nimeandika barua ya kujiuzulu kutokana na jinsi mambo yanavyokwenda, sikufurahishwa nayo. Nimeamua kujiuzulu na tayari nimekabidhi barua kwa uongozi wa Yanga, kama watapitisha nahitaji wanikamilishie stahiki zangu,” Van Pluijm amenukuliwa na chanzo cha habari hii.
Wakati huohuo, mzambia George Lwandamina amesema hajasaini mkataba wowote na Yanga ingawa amekiri Yanga inamuhitaji.
Amesema kwamba, kama watakubaliana yupo tayari kuja na kuipa Yanga mafanikio zaidi.
0 comments:
Post a Comment