Friday, August 12, 2016

Mwanamuziki Bow Wow kustaafu akiwa na miaka 29





Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za 'hip hop' Bow Wow, ambaye jina lake halisi ni Shad Moss, ametangaza kuwa atastaafu kutoka kwenye fani ya muziki, akiwa na umri wa miaka 29, mwaka huu 2016.
Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.
Bow Wow alitoa albamu yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 13, mwaka 2000.
Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni "Like You" akimshirikisha Ciara na "Let me hold you" akimshirikisha Omarion.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com