HUMUD AFUATA NYAYO ZA NGASSA, UHURU, ASAINI AFRIKA KUSINI
KIUNGO wa zamani wa Ashanti United, Mtibwa Sugar, Simba SC na Azam FC amesaini mkataba wa mwaka mmoja katika timu ya Real Kings FC. Humud ambaye alikuwa nahodha wa Coastal Union ya Tanga ambayo iliteremka daraja msimu uliopita amejiunga na timu hiyo ya daraja la kwanza Afrika Kusini kama mchezaji huru.
“Ni kweli nimesaini Kings,” anasema mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo wa kati ambaye alitabiriwa mambo makubwa wakati akichipukia Ashanti mwaka 2007.
“Nina mategemeo makubwa ya kufanya vizuri na kuisaidia timu yangu kupanda ligi kuu msimu ujao.” anasema Humud ambaye alipiga mpira wa kiwango cha juu mno wakati Taifa Stars ilipocheza na timu za Taifa za Ivory Coast na Brazil mwaka 2010.
Sasa anakuwa mchezaji wa tatu Mtanzania anayecheza Afrika Kusini akifuata nyazo za Mrisho Ngassa na Uhuru Suleimani Mwambungu.
0 comments:
Post a Comment