Saturday, October 17, 2015

SUNDERLAND LAUNCH SPORTS CENTER IN TANZANIA


 
Klabu ya soka ya Sunderland ya England mwishoni mwa wiki hii wataandika historia katika sekta ya michezo barani Afrika na hasa katika nchi ya Tanzania.
Klabu hiyo itafungua kituo cha hifadhi ya michezo kwa vijana wadogo kituo hicho kilipo eneo la kidongo chekundu Jijini Dar es saalam.
Kituo hicho kitatoa huduma za kimichezo, kielimu na afya kwa wanamichezo chipukizi wanaochipukia nchini Tanzania.
Timu ya Sunderland imeshirikana na kampuni ya kuzalisha umeme ya Marekani ya (Symbion Power) kutengeza sehemu hiyo ya michezo itayokua ikiitwa JMK Youth Park.
kirefu cha jina la kituo hicho ni JMK, ni jina la Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkurugenzi wa Sunderland Margaret Byrne, ameiambia BBC wanatarajia kituo hicho cha michezo kitawasaidia wanamichezo wachanga wa kizazi cha sasa kuendeleza vipaji vyao.
Kituo hicho kina viwanja vitatu vya nyasi bandia, kiwanja kimoja cha mchanga, viwanja viwili vya mchezo wa mpira wa kikapu, huku kukiwa na taa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya michezo ya usiku.
Uzinduzi wa hifadhi hiyo ya michezo ni mpango ulipo kati klabu hii ambayo pia inafahamika kama Black Cats na bara la Afrika katika kufundisha makocha, wachezaji wadogo na kuzijengea uwezo timu za barani Afrika.
Mahusiano ya klabu hii na bara la Afrika yalianza mwaka 2012 walipopata udhamini wa kampuni ya mafuta ya Tullow.
Sehemu ya makubaliano ya mkataba huu ilikua ni kuitangaza Afrika ambapo jezi ziliandikwa "wekeza Afrika” na huu ndio utafauti wa kalabu hii na vilabu vingine vya ligi ya England vinavyowekeza katika nchi za China na Marekani.
Kuna watu zaidi ya milioni 200 kutoka ukanda wa jangwa la Sahara, wanafuatilia ligi kuu ya England.
Pamoja na kutokua timu maarufu sana barani humu lakini timu hii inaendeleza miradi ya kijamii katika nchi za Ghana, Zambia, Afrika Kusini na Tanzania kusaidia kufundisha mpira katika ngazi ya chini.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com