Wednesday, November 16, 2016

Seongam na Serengeti Boys za Toshana Nguvu



Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 Serengeti Boys, jana imelazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji Seongnam FC katika ziara yake ya Korea Kusini.
Serengeti ambayo iko huko kwa mwaliko wa Shirikisho la Soka la Korea Kusini, itarejea wiki ijayo na kucheza mchezo mwingine wa dhidi ya nyota 40 walioteuliwa na Airtel baada ya michuano ya Kampuni hiyo ya simu.
Serengeti Boys imepata nafasi hiyo kutokana na umahiri wake wa kucheza soka la ushindani kwani kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, imeweza kucheza michezo 16 ya kimataifa ambako imekuwa ikifanya vema katika mechi 15 kabla ya 16 iliyopoteza dhidi ya Congo-Brazaville katika michuano ya kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com