Thursday, October 27, 2016

Wakala wa Farid Musa akanusha kupatikana kibali cha kazi, mchakato bado unaendelea




UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuwataarifa wapenzi wa soka kuwa winga wao Farid Mussa, leo amepata kibali rasmi cha kufanya kazi nchini Hispania.
Kwa muda mrefu Azam FC imekuwa ikisubiria kibali hicho ili mchezaji huyo akaanze maisha mapya ya soka nchini humo katika timu ya Deportivo Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Kufuatia kibali hicho kupatikana, Mussa anatarajia kuondoka nchini muda wowote kuanzia sasa kwenda kuitumikia timu hiyo.
Tunapenda mashabiki wa soka watambue kuwa Mussa anakwenda Tenerife kwa kwa makubaliano maalumu ya pande zote mbili ukiwa ni usajili wa mkopo na Azam FC itanufaika kupitia uhamisho wake mwingine atakaposajiliwa kwenda timu nyingine barani humo.
Tunaamini uwepo wake kwenye klabu hiyo utafanikisha kukuza kipaji chake zaidi pamoja na thamani yake kwa ujumla, ukizingatia bado ni mchezaji kijana anayeendelea kujifunza.
Kabla ya kibali hicho kutoka, kuna taarifa mbalimbali zilizotolewa zikiihusisha Azam FC kuwa tumemzuia kijana wetu huyo kujiunga na timu hiyo, lakini inaomba ieleweke kuwa kibali kilichotolewa leo hii ndicho kilichokuwa kikikwamisha uhamisho huo na tunamshukuru Mungu kimepatikana.

Tunaomba ieleweke kuwa, Azam FC haitafanya jitihada zozote za kuziba milango ya wachezaji wetu pindi watakapopata timu nje ya nchi, sisi tutakuwa wa kwanza kuwaongoza katika kufikia malengo yao makubwa ya kucheza soka la kulipwa kwenye maslahi mazuri endapo taratibu za usajili zitafuatwa.
Azam FC tunapenda kuishukuru Tenerife kwa kufanikisha uhamisho huo na tunamtakia mafanikio mema Mussa katika maisha yake mapya ya soka na tunaamini ataitangaza vilivyo timu yetu kimataifa na Tanzania kwa ujumla jambo ambalo litafungua milango kwa wachezaji wengine kuungana naye huko.

Imetolewa na Uongozi wa Azam FC

Jana usiku Azam TV kupitia kipindi cha MSHIKEMSHIKE VIWANJANI walithibisha kupatikana kwa kibali cha kazi cha kiajana Farid Musa kwa ajili ya kwenda kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Tenerife ya nchini Hispania, lakini General Manager wa Azam FC Abdul Mohamed alisikika kwenye radio akithibisha kupokea kibali cha kazi cha winga huyo ambaye kwa sasa hajacheza mechi yoyote ya kiushindani tangu kuanza kwa ligi akisubiri safari yake kuelea Ulaya.

Wakala wa Farid Musa, John Sorzano amekanusha habari zilizozagaa kuwa tayari kibali cha kazi kimeshatoka na badala yake amesema hicho kilichotapakaa kwenye mitandao ya kijamii si kibali ni form ambayo itatumiwa katika mchakato wa kuombea kibali.
Solzano ameshangaa form hiyo kutapakaa mitandaoni wakati ni kitu cha siri huku akisisitiza kuwa, wametumiwa Azam na yeye lakini kwa upande wa Tanzania, tayari form hiyo imeshaonekana kwenye mitandao ya kijamii. Kitendo cha hiyo form kusambaa mitandaoni huenda kukahatarisha Farid kupata kibali cha kazi.
“Hii form nimetumiwa mimi pamoja na klabu ya Azam, lakini nashangaa wao wameiweka mitandaoni wakati ni kitu cha siri, kwa upande wangu mimi nilifanya kuwa siri. Farid sio kwamba amepata kibali lakini mchakato bado unaendelea,” anasema John Sorzano wakala wa Farid Musa.

“Kitendo cha kuitoa form hadharani ambayo ni document ya serikali kinaweza kikahatarisha mchakato kwasababu ikumbukwe Tanzania pia kuna ubalozi wa Hispania ambao unaweza kuona yanayofanyika kwenye mitandao ya kijamii wanaweza wakahoji kwanini document hiyo imesambaa hivyo, inaweza kuleta ugumu.”

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com