Monday, August 22, 2016

Hiki ndicho chanzo cha bifu la Vera na Huddah




Mrembo kutokea pande za Mombasa nchini kenya, Vera Sidika ametoa sababu ya kuwa na bifu na mlimbwende mwenzake wa nchini humo, Huddah Monroe, bifu ambalo limeteka vyombo vya habari kwa muda mrefuAkifunguka kwenye Maojiano FNL ya East Africa Tv na Radio, Vera Sidika amesema wakati yeye akiwa Mombasa, Huddah Monroe tayari alishakuwa maarufu jijini Nairobi, lakini alipoenda ingawa walianza kwa kuwa marafiki, lakini baadaye Huddah alionyesha kutopenda uwepo wa Vera jijini Nairobi, kwani alihisi anamchukulia nafasi yake kwenye kazi.

"Bifu ambayo yeye anayo ilikuwa yeye amekuwa Nairobi na tayari alishakuwa star, na mimi nikatoka Mombasa nikaja Nairobi, ikawa kama nimeingilia career yake, ikawa anaaza bifu leo, anaanza kesho sasa inachosha, sasa mi nasemaga mambo kama hayo sitaki lakini anayaleta tu", alisema Vera Sidika.
Vera aliendelea kusema kuwa kitendo hicho yeye hakipendi, hasa pale inapofikia hatua ya kuchafuana kwenye mitandao kwa kutoleana habari za uongo, akitolea mfano wa hivi karibuni wa Hudda kumtangaza kuwa yeye ni muathirika wa Ukimwi.

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com