MKE WA WAZIRI MKUU MSTAAFU APATA AJALI...
Mke wa waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda, mama Tunu Pinda amepata ajali akitokea mkoani Dodoma baada ya gari aliyokuwa akisafiria kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki na kupinduka na kusababisha kifo cha mwendesha pikipiki papo hapo katika eneo la Mkundi, barabara kuu ya Morogoro Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro, ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutegwe amesema ajali hiyo imehusisha gari aina Land Cruser lenye namba za usajili STK 9442 lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea jijini Dar-es-salaam lililokuwa limembeba mke wa waziri mkuu mstaafu mama Tunu Pinda, ambapo imepinduka ikijaribu kumkwepa.
Mwendesha pikipiki aliyetokea njia ndogo na kuingia ghafla barabara kuu bila kuchukua tahadhari, ambapo watu wanne akiwemo mama Pinda, mlinzi wake Bi Gaudensia Tembo, dereva wa gari hilo Angelo Mwisa na ndugu wa mama Pinda, Gilbert Sampa ambaye ameumia sehemu ya kifua.
Akizungumzia hali za majeruhi,mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dkt. Rita Lyamuya amesema hali zao zinaendelea vizuri na wanapatiwa matibabu na baadaye wataruhusiwa kuendelea na safari kuelekea jijini Dar-es-salaam
Mtu mmoja amefariki na wanne kujeruhiwa akiwemo mama Tunu Pinda katika ajali ya gari iliyotokea leo mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment