Friday, February 26, 2016

MBWAA KUTOKA MAREKANI WA UKAGUZI WAWASILI DAR..






Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam unawakaribisha wanachama wapya wa timu ya mbwa maalumu wa ukaguzi (Canine Detection Team Tanzania) #‎CanineDetectTZ Katika kipindi cha kiangazi cha mwaka jana maafisa wa polisi wa Kitanzania wanne walikwenda nchini Marekani kwa ajili ya mafunzo maalum katika Chuo cha Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani jijini El Paso huko Texas. Katika mafunzo hayo maafisa hao pamoja na mbwa wao walipewa mafunzo ya kubaini bidhaa zitokanazo na wanyama pori zinazovushwa kimagendo na madawa ya kulevya. Maafisa hao na mbwa wao waliungana tena jijini Dar es Salaam wiki iliyopita kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo katika eneo lao la kazi. Fuatilia ukurasa wetu wa Facebook katika wiki zijazo ili kufahamu Zaidi kuhusu mbwa hao na programu hii mpya!

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2015 Dar One
| Distributed By Hotrootnews.blogspot.com