Msaidizi wa Lowassa achunguzwa uraia wake
Maafisa wa polisi nchini Tanzania
wamesema kuwa wanamzuia msaidizi wa aliyekuwa waziri mkuu wa taifa hilo
Edward Lowassa ili kuchunguzwa kuhusiana na uraia wake.
Kulingana
na gazeti la The Citizen nchini humo,wamesema kuwa bwana Bashir Fenel
Awale Ally ambaye amekuwa mtu muhimu katika kampeni za urais za bwana
Lowassa atachunguzwa kuhusiana na stakhabadhi zinazotilia shaka kuhusu
uraia wake.Kamanda maalum wa polisi katika eneo la Dar es Salaam, Suleiman Kova amewaambia waandishi wa habari kwamba stakhabadhi alizokamatwa nazo zinatatiza kuhusiana na taifa analotoka.
Amesema kuwa wakati wa kukamatwa kwake mtu huyo alipatikana na cheti cha kuzaliwa kinachoonyesha kwamba alizaliwa tarehe 11 mwezi Julai mwaka 1969 mjini Dodoma.
Kulingana na afisa huyo mshukiwa huyo pia alipatikana na pasipoti iliotoka jijini nairobi na ambayo inayoonyesha kwamba alizaliwa mjini humo mnamo tarehe 11 mwezi Julai mwaka 1969,akiwa na jina la Bashir Fenal Abdi Ally Awadhi .
Mshukiwa huyo anayedaiwa kuwa mwanaharakati na mfuasi mkubwa wa chama cha upinzani Chadema alikamatwa nyumbani kwake huko Mikocheni.
Kova amesema kuwa kuna ishara kwamba mshukiwa huyo ni raia wa Kenya.
Ameongezea kuwa sheria za Tanzania haziruhusu mtu asiye raia wa taifa hilo kushiriki katika maswala ya kisiasa ikiwemo kushiriki katika kampeni na kupiga kura.
0 comments:
Post a Comment