Serikali imeanza mchakato wa kuagiza mabasi mapya 165 ya mwendokasi
yatakayotoa huduma za usafiri kwa wakazi Dar es Salaam kwenye maeneo
yasiyo na huduma hiyo.
Tayari imeshatangaza zabuni ya kununua mabasi hayo na mwezi Desemba, mwaka huu itasaini mkataba na mzabuni.
Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), Ronald Rwakatare
amewaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa na Tawala za
Mikoa waliotembelea mradi huo kuwa wanatarajia mabasi hayo yataanza kazi
Aprili mwakani.
“Mabasi haya yatahudumia maeneo ya Morocco, Tegeta, Masaki, Makumbusho
na mengine yasiyofikiwa, wakati tukiendelea na ujenzi wa awamu ya pili
ya mradi huo,” amesema.
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 22 Agosti, 2016
amepokea taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha
kusindika gesi asili (LNG Plant) kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la
Likon'go, Mchinga Mkoani Lindi.
Mwakilishi
Mkazi wa Kampuni ya Statoil ya nchini Norway ambayo ni moja ya Kampuni
zitakazowekeza katika mradi huo Bw. Oystein Michelsen amemueleza Rais
Magufuli kuwa ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kugharimu Dola za
Kimarekani Bilioni 30 sawa na zaidi ya Shilingi Trilion 65 za Kitanzania
na kwamba uzalishaji unatarajiwa kuchukua muda wa zaidi ya miaka 40
baada ya kuanza.
Bw. Oystein Michelsen amebainisha kuwa Serikali ya Norway ina dhamira
ya dhati ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa manufaa ya pande
zote na ameomba Serikali ya Tanzania iendelee kutoa ushirikiano ili
kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho.
Kwa upande wake Rais Magufuli amemuhakikishia Mwakilishi huyo wa
kampuni ya Statoil kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kuhakikisha
mradi unafanikiwa na ameitaka Wizara ya Nishati na Madini kupitia
Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kushirikiana na wadau kutoka
Wizara nyingine kuharakisha mchakato wa kuanza kwa ujenzi wa kiwanda
hicho.
"Nataka kuona mradi huu unaanza kujengwa, tunachukua muda mrefu mno,
kamilisheni mambo yaliyobaki ili wawekezaji waanze kazi mara moja"
Amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amesema mradi huo unatarajiwa kuzalisha ajira kwa idadi
kubwa ya watanzania na utaiwezesha serikali kupata mapato kupitia tozo
mbalimbali, na hivyo kutumika kuimaisha huduma za kijamii zikiwemo
elimu, afya, maji na miundombinu.
Pamoja na Statoil kampuni nyingine zinazoshiriki katika uwekezaji wa mradi huu ni Shell, Exxon Mobil, Pavillion na Ophir
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) nao umesema unatarajia
kufanya "maandamano ya amani" nchi nzima Agosti 31 kwa ajili ya kueleza
utendaji kazi bora wa Rais Dkt. John Magufuli kwa watanzania.
Wakati
Jeshi la Polisi nchini likiwa limepiga marufuku maandamano ya nchi
nzima yaliyotangazwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hii
leo Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) nao umesema
unatarajia kufanya "maandamano ya amani" nchi nzima Agosti 31 kwa ajili
ya kueleza utendaji kazi bora wa Rais Dkt. John Magufuli kwa watanzania.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema tayari
wameshamwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata
kibali cha maandamano hayo na ulinzi huku akiwaeleza wandishi wa habari
kuwa kiu yao ni kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji wa Rais
Dk. Magufuli katika kushamirisha dhana ya maendeleo na kuleta mageuzi ya
kiuchumi.
Maandamano hayo yataanzia katika ngazi za wilaya yataanzia kwenye
ofisi za UVCCM ngazi ya
wilaya na mkoa na kuishia katika ofisi za wakuu
wa wilaya na mikoa huku wanachana wa vyama vingine na wapenda maendeleo
wakikaribishwa kujiunga na maandamano hayo ya amani.
Mkutano
Mkuu Maalum wa Chama Cha Wananchi (CUF), uliofanyika jana jijini Dar es
Salaam ukilenga kuwachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa chama
hicho ulivunjika baada ya wajumbe kuanza kurushiana viti na matusi baada
ya kupishana katika hoja ya kumtosa aliyekuwa Mwenyekiti wake, Profesa
Ibrahim Lipumba.
Profesa
Lipumba alijiuzulu nafasi yake kabla ya kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka
jana akieleza kuwa roho inamsuta kumnadi mgombea urais aliyeungwa mkono
na vyama vya Ukawa. Lakini mwaka huu alirejea na kuandika barua akiomba
kurejea kwenye nafasi yake hali iliyozua sintofahamu.
Taarifa
kutoka ndani ya Mkutano huo zimeeleza kuwa wajumbe 832 walihudhuria
lakini hoja ya kumjadili Profesa Lipumba ilipofikiwa, baadhi ya wajumbe
ambao wanamuunga Mwenyekiti huyo wa zamani walizua vurugu wakipinga
utaratibu uliotumika.
Baadhi
ya wajumbe hao waliwaambia waandishi wa habari kuwa viongozi waliopo
madarakani walifanya ubabe kwa kulazimisha kura ya kukubali au kukataa
ombi la Lipumba ipigwe kwa uwazi na sio siri kama Katiba inavyoeleza.
“Haki
haikutendeka, ni ubabe. Wala mkutano haikuzingatia kutimia kwa akidi.
Tulilazimishwa kupiga kura kwa kunyoosha mikono wakati mazingira
yaliyopo na usahihi, kura ni siri,” mmoja wa wajumbe hao alikaririwa.
Baada
ya kupiga kura za wazi, Lipumba alipata kura 14 kati ya kura 832 hivyo
kuonekana kukataliwa kwa kishindo, lakini vurugu zilizuka ghafla
kutokana na maamuzi hayo na mkutano ukashindwa kufanikisha zoezi zima la
kuwapata viongozi hao wapya.
Katika
hatua nyingine, Juma Haji Duni alijiengeu katika kinyang’anyiro cha
uchaguzi huo, baada ya baadhi ya wajumbe kusisitiza kuwa katiba inamtaka
mtu aliyejiuzulu na kuhamia chama kingine kusubiri miaka miwili ili
agombee nafasi ya uongozi ndani ya chama pale atakaporejea.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi na Mipango wa CUF, Shaweji Mketo, alisema kuwa Duni
alijiondoa kutokana na maadui wa Ukawa kutaka kukihujumu chama hicho.
Mkutano huo umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena.
Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki EADB imezitaka nchi za kanda
hiyo kuboresha sheria kwenye sekta ya uchimbaji madini ili kuhakikisha
rasilimali zinapangwa kwa usawa.
Akiongea kwenye semina ya kikanda
ya majaji kutoka nchi za Afrika Mashariki iliyomalizika jana Nairobi,
Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Vivienne Yeda, amesema ugunduzi na
uchuguzi unaoendelea wa madini katika kanda hiyo umeongeza matumaini
ya kuongeza utajiri, kupunguza nakisi ya bajeti na kuboresha maisha ya
watu wa nchi hizo. Amesisitiza kuwa mafao lazima yaende kwenye jamii za
nchi husika, kwa njia za mirahaba, kodi, mgao, fursa za biashara, kazi
za kitaalamu na ajira kwa wafanyakazi wenye ujuzi.
Semina hiyo iliyoandaliwa na EADB, imewalenga majaji wa Afrika
mashariki wanaohusika na kazi ya usuluhishaji na kutatua migogoro kwenye
sekta ya madini.
Picha za bingwa wa mbio za mita 100,200 na relay kwenye mashindano
matatu ya Olimpiki Usain Bolt zimeenea kwenye mitandao ya kijamii.
Bolt anaonekana kwenye pozi za mapenzi na msichana anaedaiwa kuitwa
Jady Duarte wa umri wa miaka 20 ambae ni mwanafunzo wa chuo kimoja cha
Brazil
Inasemakana Bolt alikua
tayari kashatangaza kumuoa mchumba wake Kasi Benestt baada ya olimpiki
na huenda ndoa hiyo ikaingia doa.
Hata hivyo taarifa hizi huenda
zisimtatize sana Bolt kwani yeye amewahi kukubali kwamba hawezi kuwa na
uhusiano na mwanamke mmoja.
Siku chache baada ya Wema Sepetu na Idriss kutofautiana na Idris
kumuondokea Wema,Mwanadada huyo ameonekana kupata tabu sana na maisha
bila mpenzi wake.
Hivi kaamua kutumia mtnadao wa kijamii kumuomba msamaha.
Amesema " That moment you realise how much u miss a special someone… Rudi basi… hata kidogo tu
Licha
ya Serikali kuanzisha vita dhidi ya biashara haramu ya uuzaji mwili,
Wilaya ya Kinondoni inakabiliwa na ongezeko la biashara haramu ya ngono
kwa muda mrefu ambapo eneo la Tandale linatajwa kukithiri vibanda vingi
vya dada na kaka poa.
Wakuu
wa wilaya wengi wamepita katika wilaya ya Kinondoni pasipo kutokomeza
changamoto hiyo. Lakini Mkuu wa sasa wa Wilaya hiyo Mh. Ally Hapi
amejidhatiti kuuvunja mwiko huo. Hivi karibuni Hapi alitaja mikakati ya
kutokomeza mtandao wa biashara hiyo.
Alisema
atahakikisha anavunja vibanda vyote vinavyotumiwa na dada pamoja na
Kala poa , vilevile watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hapi
alisema amepokea idadi ya vibanda vinavyotumiwa na dada poa na kwamba
mpango wake ni kuvifunga kisha kutafuta wawekezaji ili Wamiliki wa
vibanda hivyo walipwe fidia na kupisha ujenzi wa vitega uchumi.
“Niliwaagiza
watendaji wa kata kuniletea idadi ya madanguro, nimeshajua mahali
yalipo madanguro hayo, na kwamba nitakwenda kuchukua hatua ya kufunga
madanguro pamoja na kuwapeleka dada poa mahakamani,” alisema. Alisema
hatawachukulia hatua za kisheria dada/kaka poa pekee, bali hata wamiliki
wa baa zitakazowahifadhi watu hao watachukuliwa hatua.
“Hatutashughulika na dada poa pekee bali hata Wamiliki wa nyumba na au baa watachukukiwa hatua. Hilo likitekelezwa
Kila mtu atatimiza wajibu wake,
nimegundua wamiliki wengi wa madanguro hawapo hapa na idadi ya madanguro
katika eneo la Tandale pekee kuna vibanda 58.” alisema.
Alisema
utekelezaji wa ubomoaji nyumba umeshaanza kujadiliwa na kwamba
wanasubiriwa wawekezaji ili wapewe fursa za kujenga maduka na vitega
uchumi.
“Tunataka wenye fedha zao waje wawekeze ili tuwalipe fidia wenye nyumba, zibomolewe,” alisema na kuongeza.
“Huu mfupa uliwashinda watangulizi wangu lakini mimi nitautafuna.”
Kuhusu
baa zinazokiuka sheria, alisema atawaondoa watendaji wa kata waliokaa
muda mrefu kwa sababu wengi wao ndiyo chanzo cha ukiukwaji wa sheria.
“Watendaji
waliokaa muda mrefu waondolewe sababu tumegundua hushirikiana na wenye
baa kupiga kelele, wanachukua fedha zao na kuwaacha kupiga kelele usiku
wa manane kinyume cha tarabibu,”
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi amewapiga marufuku mgambo wa
wilaya hiyo kuwafanyia fujo wafanyabiashara wadogo wanaofanya shughuli
zao katika maeneo rasmi.
Hapi aliyasema hayo jana katika kipindi cha Mada Moto kinachorushwa moja kwa moja na kituo cha Channel Ten.
Alisema
kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu kuwatoza ushuru kinyume cha
sheria wafanyabiashara hao wanaofahamika kwa jina la wamachinga jambo
linalosababisha halmashauri ya manispaa ya kinondoni kupoteza mapato.
“Kuna
mtu mmoja alikuwa anatoza wamachinga ela, zaidi ya sh 8,000 kwa siku na
walikuwa wanalipa, kama serikali ikiweka mfumo mzuri inaweza kupata
mapato ya uhakika kutoka kwa wamachinga,” alisema.
Alisema
atahakikisha anapata idadi ya wamachinga wote katika wilaya hiyo ili
kuwawezesha kiuchumi ikiwemo kuwapa mikopo na kutenga siku ya gulio ili
wapate fursa ya kufanya biashara.
“Machinga
wote tuwatambue tuwaunganishe na bima ya afya, wapewe mikopo hakika
watainuka sababu hakuna mtu aliyezaliwa kuwa machinga muda wote,
tunataka Kuwainua ili waje kuwa wafanyabiashara baadae,” alisema.
“Ni marufuku kupiga na kuwasumbua wamachinga, kuwaibia bidhaa zao ni marufuku,” alisema.
“Sisi
viongozi kazi yetu ni kuwaongoza na kuwaonyesha Mahala panapostahili
wao kufanyakazi, na wilaya yangu ya kinondoni ina mkakati wa kuandaa
magulio ili wafanyabiashara ndogondogo wauze bidhaa zao, ” alisema.
Aliongeza
kuwa “Nyuma kulikuwa na mianya ya upotevu wa mapato, tumefanya kazi
kubwa Na kamati ya usalama na sasa watu wanafurika kulipa kodi. “
“Tunawaomba
watanzania watuombee kwa kuwa tunaopambana nao siyo wote wanafurahi.
Wananchi washiriki katika kutoa taarifa za wakwepa kodi na kadhalika,”
alisema.
Mwanafunzi
wa Chuo Robert Mfune mwenye umri wa miaka 19, ameweza kutengeneza zaidi
ya maelfu ya Paundi za Uingereza akiwa anafanyakazi katika muda wa
ziada kwenye mgahawa ya McDonald’s kama mhudumu.
Robert
ambae alipokua na umri wa miaka 16 tu, alianza kufanya kazi kama
mhudumu katika kampuni ya McDonalds nyumbani kwao Southampton, ambako
alipata kujifunza mambo mengi kuhusu biashara, na baadae kuanza kufanya
biashara zake mwenyewe na kuweza kutengeneza pesa za kutosha kununua
gari ya kifahari aina ya Bentley na kumnunulia nyumba ya kuishi mama
yake mzazi.
Alisema ilikua ngumu sana kwake kufanya kazi katika mgahawa ya McDonald’s, kufanya biashara zake na kusoma kwa wakati mmoja.
“Nikama
kwenda chuo na hela ya mkopo, kama utazingatia masomo na kuweka malengo
ya kufanya vizuri basi utafanikiwa”. alisema mfanyabiashara Mfune.
Mafanikio
yake yalianza baada ya kumaliza masomo yake ya chuo, na kufanya kazi
kama mhasibu katika idara ya fedha. Hivyo kumpelekea kupata ujuzi zaidi
katika mambo ya biashara, na kuanza kufanya biashara zake akitumia
akaunti zenye jina la mama yake na kuweza kupata mafanikio hayo.
“Nilipokua
mhudumu nilijitahidi kujifunza mambo kazaa hivyo nikienda nyumbani
nafanya utafiti mwenye na kufanya cha kwangu”. alisema Mfune.
Mfune
kwa sasa anafanya biashara zake kwa kutumia akaunti yake mwenyewe, huku
pia akiwa ameweza kuwekeza katika Migahawa ya chai mbalimbali mjini
Uingereza.
Pia
anamiliki magari yenye thamani ya zaidi ya Pauni 250,000£ ikiwemo Range
Rover, Bentley continental GT ya rangi ya dhahabu lakini amedai kwamba
yeye sio mtu wa kuthamini mali na magari bali utu wa watu na kujali
marafiki zake.
Serikali nchini Tanzania imelifungia
gazeti la kila wiki la Mseto kuchapishwa katika njia zote ikiwa ni
pamoja na mitandao. Hili ni gazeti la pili kufungiwa ndani ya mwaka
mmoja.
Serikali inasema Mseto limekuwa likiandika taarifa za uongo
na kugushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za serikali huku taarifa hizo
zikiwa na nia ya uchochezi na kumchafua Rais John Magufuli na viongozi
wengine wa serikali yake.
Akitangaza kufungiwa kwa gazeti hili
mapema leo hii, Waziri mwenye dhamana ya habari Nape Nnauye amewaambia
waandishi wa habari kuwa amelifungia gazeti hilo kwa mujibu wa Sheria ya
Magazeti ya mwaka 1976
Hakuna taarifa rasmi yoyote ya mwitikio wa kufungiwa huko kutoka kwa wachapishaji na wamiliki wa gazeti hilo
Hili ni gazeti la pili kufungiwa ndani ya mwaka mmoja. Mwezi Januari
mwaka huu, serikali ililifungia pia gazeti la Mawio muda wote.
Wasiwasi miongoni mwa wadau wa habari umeendelea kuongezeka kwa kile
kinachoonekana kuwa utawala huu mpya unaviminya vyombo vya habari na
kukandamiza uhuru wa kutoa na kupokea habari pia hapa nchini Tanzania.
Tayari watu wawili wameshtakiwa baada ya kuandika jumbe katika mitandao ya kijamii zilizoonekana kumtusi Rais Magufuli
Inawezekana kufungwa huku kwa gazeti la Mseto kutaibua ukosoaji hasa
kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu ambao wamekuwa wakiikosoa
Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo wanasema inatoa mamlaka makubwa
sana kwa serikali kuminya uhuru wa habari nchini
Tajiri mmiliki wa ardhi ambaye pia
amekuwa akisaidia wasiojiweza katika jamii, Mtawala wa Westminister
Gerald Cavendish Grosvenor amefariki na kumwachia mwanawe Hugh Grosvenor
urithi wa £9bn.
Alikuwa na binti watatu, na mwana mmoja pekee wa kiume, Hugh, mwenye umri wa miaka 25.
Hugh amerithi "nusu ya London" kwani ardhi nyingi maeneo mengi ya Belgravia na Mayfair, London ilimilikiwa na babake.
Yeye
hufanya kazi katika kampuni ya Bio-bean, kampuni inayoangazia
teknolojia isiyoongeza gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani.
Kwa
mujibu wa orodha ya jarida la Forbes ya mwaka 2016, kuna vijana wengine
tisa wa chini ya umri wa miaka 30 ambao utajiri wao ni zaidi ya dola
bilioni moja za Marekani.
Vijana wengine matajiri ni: 2 & 3: Alexandra, 20, na Katharina Andresen, 21
Ndio wachanga zaidi na wanamiliki kampuni ya Ferd.
Binti hawa walirithi utajiri hu kutoka kwa baba yao Johan, raia wa Norway mwaka 2007. 4: Gustav Magnar Witzoe, 23
Anatoka Norway pia na huonesha maisha yake ya kifahari kwenye Instagram.
Amerithi sehemu ya biashara ya babake ya kufuga samaki na sasa utajiri wake ni $1.1bn (£846m).
Gustav Witzoe, babake ambaye wana jina sawa, alimpa hisa kwenye kampuni hiyo kama zawadi. Lakini hana udhibiti au usemi wowote. 5&6: Ludwig Theodor Braun na dadake
Haonekani sana mtandaoni. Hayupo kwenye Twitter au Instagram lakini anatambuliwa kwa utajiri.
Familia yake ilianzisha kampuni ya dawa ya B. Braun Melsungen, Ujerumani 1839.
Kampuni hiyo ni maarufu sana kwa dawa na vifaa vya matibabu.
Ludwig humiliki 10% ya kampuni hiyo ambayo ni sawa na $1.8bn (£1.4bn).
Dadake Eva Maria Braun-Luedicke yuko nyuma yake kidogo lakini utajiri wake ni $1.4bn (£1bn).
7&8: Waanzilishi wa Snapchat
Evan Spiegel ni mmoja wa walioanzisha mtandao wa Snapchat ambao hutumiwa na mamilioni ya vijana duniani.
Majuzi, aliingia uchumba na mwanamitindo mashuhuri duniani Miranda Kerr.
Ana umri wa miaka 26 na utajiri wake ni $2.1bn
(£1.6bn), Evan ndiye mchanga zaidi miongoni mwa waanzilishi wa Snapchat
na ndiye tajiri zaidi miongoni mwao.
Mwenzake ni Bobby Murphy, 28, ambaye anamkaribia sana kwa utajiri.
Utajiri wa Murphy ni $1.8bn (£1.3bn). 9: Lukas Walton
Kwa mujibu wa Forbes, Lukas Walton, 29, ndiye anayemkaribia sana Hugh Grosvenor.
Utajiri wake ni $10.4bn, ambazo ni karibu £7.2bn kwa viwango vya sasa vya ubadilishanaji wa fedha vya sasa.
Anatoka katika familia tajiri inayomiliki Walmart (miongoni mwa kampuni nyingine), ambayo pia humiliki Asda nchini Uingereza. 10: Wang Han
Wang Han, raia wa China, anakamilisha orodha hii.
Chanzo cha utajiri wake ni urithi wa hisa za kampuni ya ndege ya Juneyao Air kutoka kwa babake Wang Junyao, aliyefariki 2004.
Junyao
alikuwa mwanzilishi wa kampuni ya Juneyao Group. Wang Han humiliki 27%
ya hisa za shirika hilo la ndege na 14% ya hisa za maduka ya jumla ya
Wuxi Commercial Mansion Grand Orient.
Utajiri wake unakadiriwa na Forbes kuwa $1.34bn.
BUNDA, MARA: Madiwani wa CCM katika jimbo la Bunda wamekataa kupokea madawati yaliyotolewa na Mbunge Ester Bulaya wa CHADEMA.
- Inadaiwa wameyakataa sababu yalikuwa yameandikwa majina ya Mbunge huyo.
Raia nchini Tanzania wameamkia habari za kushangaza kwamba taifa hilo linaunda ndege.
Gazeti
la Tanzania la Daily News limeripoti kwamba ndege hiyo aina ya
helikopta inakaribia kukamilika na kwamba habari hiyo imekuwa ikisambaa
barani Afrika kwa kasi.
Gazeti la Zambia, Observer linasema kuwa
lengo la ndege hiyo itayokuwa ikibeba watu kwa bei rahisi itakabiliana
na matatizo ya uchukuzi nchini humo.
Huku gazeti la Cameroon,
Concord likisema kuwa mradi huo ni wa kihistoria linaongezea kuwa lengo
lake ni kutengeza ndege 20 kwa mwaka.
Ndege hiyo yenye uwezo wa
kubeba watu wawili inakaribia kukamilika katika chuo cha ufundi cha
Teknolojia cha Arusha na itaanza kufanyiwa majaribio ya kuruka angani
baada ya kuruhusiwa na mamlaka ya uchukuzi wa angani nchini Tanzania
kulingana na Daily News.
WAZUNGU WAMTEMBELEA MTENGENEZAJI HELIKOPTA TUNDUMA
** Mkazi wa
Tunduma, mkoani Songwe, Adam Kinyekile (34) ambaye alikuwa
akitengeneza helikopta amepata mwaliko maalumu na wazungu kutoka Afrika
Kusini kutembelea kiwanda chao cha kutengeneza chopa.
Kijana
Kinyekile ambaye pia ni fundi magari alitumia ubunifu wake kuunda
helikopta, kitu ambacho kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, George
Mbijima akiwa mjini Tunduma alimtembelea kisha kuweka jiwe la msingi
kwenye helikopta hiyo.
Hata hivyo baada ya taarifa za kijana huyo kurushwa kwenye vyombo vya
habari , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilipiga marufuku kwa
mtu yoyote kutojihusisha na utengenezaji au ubunifu wa ndege bila
kufuata taratibu.
Onyo hilo lilionekana kumlenga Kinyekile kwa
kazi yake aliyokuwa akiifanya jambo ambalo lilimfanya asiweze kuendelea
na maboresho ya helikopta yake licha ya kudai ilikuwa imebaki kuruka.
Ndege mmoja ambaye inaaminika alitoka nchini Finland amepatikana katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda.
Ndege
huyo aina ya Osprey kwa sasa anatunzwa na maafisa wa kituo cha
kuwahudumia wanyama cha Uganda Wildlife Education Centre (UWEC).
Ndege huyo mkubwa, aina ya mwewe, aligunduliwa na maafisa wa uwanja
wa ndege katika njia inayotumiwa na ndege kupaa na kutua katika uwanja
wa huo wa Entebbe.
Isaac Mujaasi, afisa wa mauzo na mawasiliano
katika UWEC, ameambia BBC kwamba ndege huyo alikuwa ameumia katika
mabawa yake baada ya kugongwa na ndege iliyokuwa inapaa.
Alikuwa na pete yenye maelezo kumhusu mguuni ambayo inaashiria kwamba
alimilikiwa na makumbusho ya historia asilia nchini Finland.
Bw Mujaasi anasema waliwasiliana na maafisa wa makumbusho hao ambao wamethibitisha kwamba ndege huyo ni wao.
“Hili lilituthibitishia kwamba ndege huyu alisafiri kutoka Helsinki,
Finland,” Bw Mujaasi amesema. “Tutamtibu ndege huyo na akipona
tutamwachilia na huenda akarejea kwao.”
Afisa huyo hata hivyo
amesema ni kawaida kwa ndege kuhama kutoka Ulaya, hasa wakati wa majira
ya baridi na kukimbilia maeneo yenye joto.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu Nchemba hii leo amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi kubwa ikiwa
ni kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyofanywa na raia wa china
wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro-Geita dhidi ya
wafanyakazi/vibarua ambao ni watanzania.
Takribani wiki moja sasa kumekuwa hali ya sintofahamu dhidi ya picha
zinazoenezwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari zikionesha raia wa
tanzania anayefanya kazi kwenye mgodi tajwa akiteswa na kufanyiwa
vitendo vya kinyama na mwajili wake ambaye ni raia wa china.
Imemlazimu waziri mwenye dhamana na usalama wa raia na mali zao kupitia
wizara ya mambo ya ndani kufika eneo la mgodi kujiridhisha kwa taarifa
zilizotapakaa na kubeba simanzi kwa watanzania.
Mwigulu Nchemba
amejiridhisha kuwa kulikuwepo na tukio hilo la mtanzania kuteswa na huyo
mwajili wake kipigo kilichopelekea kupoteza fahamu na sio kifo.
Hatua za awali mwigulu alizozifanya ni kwenda gereza la Geita mjini
alikohifadhiwa kijana huyo kwa madai ameshitakiwa na mwajili wake kwa
kosa la wizi lililopelekea yeye kupigwa.
Katika mahojiano ya
waziri Mwigulu Nchemba na kijana huyo,Mwigulu alibaini kuwa kijana huyo
aliyepo gerezani ndiye mhanga wa tukio lile kwa uthibitisho wa makovu
yaliyopo mwili mwake na mavazi aliyovalia wakati anateswa na wakati yupo
hapo gerezani.
Katika hali hiyo ilimlazimi Mh.Mwigulu kwenda
mgodini akiwa ameambatana na kijana huyo kwaajili ya kutambua waliofanya
vitendo hivyo vya kinyama.
Katika oparesheni hiyo, kijana
aliyeteswa na kujeruhiwa aliwabaini watanzania 5 ambao ni walinzi wa
eneo hilo na mchina mmoja walioshirikiana kumpiga,kumtesa na kumjeruhi.